Pre GE2025 Dk Doto Biteko: Tujitokeze ili tuweze kugombea kwa ajili ya kuhudumia nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,116
2,161
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amewaasa Wakristo kuliombea Taifa amani, utulivu, umoja na mshikamano uendelee katika kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu imeeleza, Dk Biteko amesema hayo leo Jumapili, Aprili 20, 2025 jijini Mwanza wakati aliposhiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa la African Inland Church (AIC) - Makongoro.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Mwaka huu ni wa uchaguzi na una michakato mbalimbali ya kujiandikisha, kugombea, kupiga kura na kutangaza matokeo. Kwa niaba ya Serikali napenda kuwaomba waumini wa AICT na wale ambao tunadhani tuna uwezo wa kugombea nafasi mbalimbali tujitokeze kwa wingi tugombee, wale tu wenye nia ya kweli tuhakikishe tunawasaidia watu katika hali zao,” amesema Dk Biteko.

Sambamba na kugombea amewahimiza waumini kuliombea Taifa kuelekea wakati na baada ya uchaguzi: “Tujitokeze ili tuweze kugombea kwa ajili ya kuhudumia nchi yetu na wakati wa kampeni utakapofika naomba tuendelee kuliombea Taifa.”

Kuna muda watu wanachekesha sana
Upepo uliopo watu wanataka mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi

Biteko mgombea halafu Mkurugenzi wa halmashauri na mwalimu ndio referee na lines Men

Biteko yeye kwa sasa ana uhakika wa kushinda kisa referee na lines Men ni watu waliowateua wao

Mbona anaogopa mabadiliko ya wasimamizi wa uchaguzi na watu kuwepo kwenye vituo kusubiri kura kuhesabiwa

Kura zikipigwa kweupe yeye mwenyewe biteko hapati ubunge

Kama Biteko anajiamini amwambie boss wake wafanye Reforms ili uchaguzi uwe huru na masanduku ya kura yakae peupe kama watatoboa
 
Amani ili wale kwa amani? manina zao
 
Yaani watu anaowasimamia ndio wasimamizi wa uchaguzi.

Sisi sio kondoo kwamba uone hii ni hatari na uingie.

Msemo wa kiswahili unasema "Aliyeshiba hamjui mwenye njaa"

Haya mambo ya tume haisimami kwa haki kwao hayawezi kuwaumiza hata kidogo kwanza ndio furaha yao
 
Kuna muda watu wanachekesha sana
Upepo uliopo watu wanataka mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi

Biteko mgombea halafu Mkurugenzi wa halmashauri na mwalimu ndio referee na lines Men

Biteko yeye kwa sasa ana uhakika wa kushinda kisa referee na lines Men ni watu waliowateua wao

Mbona anaogopa mabadiliko ya wasimamizi wa uchaguzi na watu kuwepo kwenye vituo kusubiri kura kuhesabiwa

Kura zikipigwa kweupe yeye mwenyewe biteko hapati ubunge

Kama Biteko anajiamini amwambie boss wake wafanye Reforms ili uchaguzi uwe huru na masanduku ya kura yakae peupe kama watatoboa
Hapana huyu mtu chama chochote anashinda Akigombea, Amenyooka sana
 
Back
Top Bottom