Dizasta ni mdogo wa damu wa King Crazy GK aliyechagua kurafikiana na Professor Jay na Mr Ebbo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,176
DIZASTA NI MDOGO WA DAMU WA KING CRAZY GK ALIYECHAGUA KURAFIKIANA NA PROFESSOR JAY NA MR EBBO KATIKA MAKUZI YAKE.

1. Wawili hawa wana asili ya mkoa wa Mbeya lakini wamesikika zaidi wakiwakilisha Mzizima. Ununuapo kazi za Dizasta utakutana na jina Edgar MWAIPETA huku kaka yake akifahamika kwa jina la GWAMAKA linalotafsirika kama SHUPAVU, IMARA ama MWENYE NGUVU na MAMLAKA.

Wakati Dizasta amenukuliwa kuiwakilisha Tabata, kaka yake akaona sehemu poa kwake ni Upanga Mashariki.

Kuhusu huko Mbeya, D anakwambia "CHOCHORO YANGU MBEYA, YAKO NI IPI?" kwenye machochoro zote wakati GK akiitaja Mbeya kama sehemu waliko ndugu zake kwenye ngoma kama MAMA na NITAKUFAJE.

2. Wawili hawa wametokea kwenye familia kubwa za Rap zilizokuwa na vichwa vilivyofanya MAAJABU yao pia. Wakati kaka mtu akiwa na East Coast Team na vichwa kama; Mwanafalsafa, AY, Snare, Buff G, Sheriff na wana wengine kibao, mdogo mtu alikuwa na Panorama authentic na vichwa kama Dubo lakini pia alikuwa TAMADUNI Music na mabalaa kama Nikki Mbishi, One, Stereo na mabalaa kibao yasiyohitaji kuongelewa kwa kina.

3. Wawili hawa wamenyooka na WATAYARISHAJI wao maalum badala ya kurekodi sehemu tofauti. GK alifanya kazi na Master Jay, Papa Love, Joh Mahundi na Prof. Ludigo, kabla ya miaka ya baadaye kufanya kazi zaidi na Effector wa Serious Records wakati Dizasta alifanya kazi na akina Hemed Ngwesa pale TM lakini kwa sasa anafanya kazi zaidi na Ringle Beats, Jcob na Smart J Wonder.

4. Wawili hawa wamejichagulia maeneo makuu matatu ya kuyaongelea na KUONeshA umwamba wao hapo kuliko maeneo mengine.

Wawili hawa wamechagua usimuliaji wa visa; Sister Sister, Sauti ya Manka, Kosa langu, kutoka kwa Gk na Shahidi, Kikao na migoma MINGI kutoka kwa D inathibitisha hili kiasi akafikia kusema kwamba he has taken story telling to the whole new level. Na haipingiki.

Wawili hawa wamechagua majigambo
Msikilize Gk kwenye Komaa Nao, Ama Zangu ama Ama Zao, Fire halafu njoo kwenye mfululizo wa Nobody is safe kutoka kwa D
Wawili hawa wamechagua kufanya nyimbo za jamii. Sikiliza Wapi Tunaelekea, Saa Mbaya, na Tanzania kutoka kwa Gk halafu sikiliza Wengi Wao kutoka kwa D.

Wawili hawa wamejishughulisha sana na dhamira ya kifo. Wakati Gk akimkumbuka D Rob kwenye Tunakukumbuka, akaja na Nitakufaje na Tell me why AKIWA na Ay huku D akiongelea kifo kwenye karibia nusu ya ngoma zake lakini kwa UPEKEE nitaje; Siku Nikifa.

Wawili hawa wamechagua kumwongelea mwanamke kwa namna chanya sana. Msikilize Gk kwenye ngoma zake mbili za MAMA halafu njoo kwa Dizasta na Muscular Feminist

5. Wawili hawa wanaflow kwa Kiingereza, wanaflow kwa Kiswahili. Hata Jigga hawawezi, wanaflow kwa lugha mbili.

6. UPEKEE WA mitindo yao ya kughani. GK alifananishwa sana na Dark Man X (DMX) na alihoji kuwa SIKU AKIFA, NANI ATAKOPI STYLE YAKE NA KUIENDELEZA huku D akifananishwa na Shaulin Flow japo yeye anasema mtindo wake umewapa HAMASA wengi wao kama; Young Killer, Stamina, Manengo, na Boshoo.
MUHIMU; SIJATAKA KUONGELEA TOFAUTI ZILIZOPO BAINA YAO

KICHWA CHA MAKALA HII KIMETOKANA NA MAHOJIANO AMBAYO D ALIFANYIWA NA KUWATAJA PROF NA MOTIKA KAMA WATU WALIOTIA CHACHU KWENYE GAME YAKE.

RUKSA KUONGEZA UFANANO BAINA YA WAWILI HAWA
RUKSA KUKOSOA NA KUPONDA
1716977608174.jpeg
1716977620244.jpeg

LUAH
100524.
 
Sema aina ya muziki aliouchagua Dizasta, kwa bongo una wafuasi wachache sana.

Hata kazi zake ukiangalia kwenye digital platforms nyingi number hazisomi vizuri na kwenye show ni ngumu kusikia jina lake.

GK alikuwa super star wa daraja la juu linaloelekeana na wasanii kama Prof Jay au Afande huku akilibeba kundi zima la East Coast kwa kutoa ngoma zinazobamba masikioni mwa wengi.
Binafsi nazielewa kazi kadhaa za D ila ameshindwa kuifikia hadhira kubwa.

Hitimisho, mshaurini D aboreshe sanaa yake iendane na mahitaji ya walaji walio wengi kuliko kuibakiza sanaa yake mafichoni.
Kwa hatua aliyonayo ni ndogo sana kiasi cha kumkosea heshima GK kwa kufananishwa na wachanga wanaotafuta kutoboa bila mafanikio licha ya kuwepo kwenye game kwa miaka kadhaa sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom