Pre GE2025 Diwani wa kata ya Zingiziwa: Nipo tayari kukosa udiwani kuliko kushuhudia Jerry Slaa anakosa Ubunge katika uchaguzi ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Sep 2, 2024
1,715
4,455
Huko CCM nikadhani uchawa ni kwa mwenyekiti wao tu kumbe hadi wabunge sasa hivi wanafanyiwa uchawa?

Madiwani mmekuwaje lakini?

========================================

Diwani kata ya Zingiziwa, Maige Maganga amewataka Viongozi na Wananchi wa Zingiziwa na Jimbo la Ukonga kwa ujumla kujivunia uongozi wa Mbunge wao, Mheshimiwa Jerry Silaa kutokana na maendeleo makubwa aliyoyaleta katika jimbo hilo tangu awe Mbunge.

Diwani Maige ameenda mbali zaidi na kusema yupo tayari yeye akose Udiwani uchaguzi ujao lakini hayupo tayari kushuhudia Jerry Silaa akikosa ubunge katika uchaguzi ujao wa mwaka huu.

“Nani kama Jerry Silaa? Nawaapia nipo tayari kuona nakosa udiwani kuliko kushuhudia Mheshimiwa Silaa anakosa Ubunge katika uchaguzi ujao” Maige Maganga, Diwani Zingiziwa.


 
Back
Top Bottom