Diwani Selungwi asema SHIMWATA ni mgeni mwema Mkuranga

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
84
118
Diwani wa Kata ya Mbezi, Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani, Rashid Selungwi ameumwagia sifa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIMWATA) kuwa ni wageni wema Kijijini Mwanzega, zilipo nyumba za Wasanii, wanamichezo na Waandishi wa Habari.

Wema wa Shiwata kijini hapo ni kuendeleza maendeleo ya jamii na kutokuwa na mambo ambayo yanaharibu taswira ya nchi yetu.

Akizungumza katika uzinduzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi (CCM), Gomapembe-Mwanzega, Selungwi alisema wamewakaribisha vizuri Shiwata kijijini hapo na kuwataka kushirikiana naye kwa mipango ya maendeleo yatakayosaidia jamii.

Selungwi alisema pamoja na kuwataka Shiwata wakae meza moja ili kupanga mipango ya maendeleo, pia ameiomba jamii kuchangamkia fursa kijijini hapo.

Selungwi aliwataka vijana wenye elimu ya juu kuwa karibu naye ili wachakate maarifa waliyoyapata na kuyafanyia kazi kwenye uwekezaji.

Alisema vijana wasomi wanatakiwa kuacha kulalamika na badala yake, wachangamkie fursa zilizopo Mbezi na kuzifanyia kazi.

"Inashangaza vijana waliomaliza vyuo vikuu, wanalalamika hakuna ajira, wakati huku Mbezi kuna fursa lukuki, sisi tunahitaji sana maarifa mliyoyapata ili tupige hatua kimaendeleo," alisema Selungwi.

Aidha, Selungwi aliwaomba vijana wenzake kuelekea kijijini hapo kwani ndio mjini inayokuja kwa sababu ya ukaribu wa bahari na fursa nyingine zilizoko.

"Njooni tupange mipango wahitimu wa vyuo vikuu, tunahitaji maendeleo sisi," alisema.

Katika hafla hiyo, diwani huyo aliahidi kuchangia matofali 500 na mifuko mitano ya saruji kwa lengo la kujenga ofisi ya tawi la Gomapembe.

Huku Diwani wa Viti Maalum, Fatuma Mfaume aliahidi kuchangia mifuko 10 ya saruji na mchanga lori moja.

Naye, Katibu Mkuu wa Shiwata, Michael Kagondela alimweleza diwani huyo kwamba watarajie ushirikiano zaidi kutoka kwao.

Katika hafla hiyo kulikuwa na matukio kadhaa ya sanaa kutoka kwa wasanii kutoka Shiwata, zoezi la ukataji keki na mashairi.
WhatsApp Image 2024-06-24 at 11.57.59_29d84c90.jpg
 
Back
Top Bottom