Disinfectant za Neo Life, wizara ya afya, TBS na TFDA. Mko wapi kulinda afya za wana Tanzania

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
8,573
23,477
Wasalaaam.
Mheshikiwa Raisi wa Tanzania, waziri wa afya, na mamlaka husika za afya naomba mpitie hii uzi

Leo kuna jamaa yangu kanionyesha bidhaa zake anazouza NeoLife. Ila nimegundua kuwa bidhaa hizi zinaweza kuleta matatizo makubwa ya afya nchini.

Kwa sababu gani? Mfano hii bidhaa ya disinfectant, Je imethibitishwa na TFDA?
hq720.jpg

Mnaweza kuona hiyo bidhaa hapo juu ya CARE DISINFECTANT wanaouza wanadai inatibu:
  1. UTI Sugu
  2. Kutibu vidonda vya sukari na cancer
  3. Inakaza misuli ya uke iliyolegea
  4. Inaoshea mboga za majani kabla hujazipika
  5. Inatoa harufu mbaya ukeni
  6. Kusafisha masink ya choo na kufanyia usafi nk
Screenshot_20241011_231349_Facebook.jpg
Screenshot_20241011_231317_Facebook.jpg
Screenshot_20241011_225101_Facebook.jpg

Mnaweza kuona maelekezo haya kupitia kurasa za Instagram au Facebook. Je ni kweli dawa hii inafanya kazi zote hizi?

Dawa ina tahadhari: inasema kuwa isiingie machoni, usinuse, inaathari ikitumiwa mda mrefu kwenye mwili.

Mfano nimepiga picha tahadhari ya dawa ya kunywa. Ambayo wanaouza wanadai inatibu vitu mbalimbali. Ila nyuma ya dawa imekana kuwa haitibu, wala haijathibitishwa.

unaweza kuona mstari wa mwisho wameandika. THESE STATEMENTS HAVE NOT BEEN EVALUATED BY FOOD AND DRUG ADMINISTRATION. THIS PRODUCT IS NOT INTENDED TO DIAGNOS, TREAT, CURE OR PREVENT ANY DISEASE.
Screenshot_20241011_233220_Gallery.jpg


Je mamlaka husika wanaruhusu vipi watu kuuza vitamins, zikiuzwa kama kinga za magonjwa huku tahadhari wanaozalisha wanakataa hii sio dawa wala kinga?

Nje ya kifungashio kuna picha ya sink. Je watu wanaosugulia sehemu zao za siri, na kusugua ndani wakiamini inakaza misuli ya uke, ina madhara gani ya mda mrefu?

Wanawake wanashauriwa wapake hii dawa ukeni kisha walale nayo asubuhi wanaosha. Hii ni hatari sana kwa afya za watanzania kwa ujumla.

Swali langu la mwisho kwa TFDA na TBS. Kwa nini dawa ambazo hazijathibitishwa na mamlaka za afya zinatumika kuuzwa kama Tiba ya baadhi ya magonjwa huko mtandaoni.?

Hii ni bidhaa moja tu, kuna bidhaa nyingi, nyingime za kuongeza nguvu za kiume, ambazo ni hatari sana kwa afya ya mwanadamu. Tafadhali sana walengwa usika wa kusimamia haya mfanye kazi zenu.

Asanteni sana.
 
Back
Top Bottom