Costancia Adauthy
Member
- Apr 19, 2024
- 7
- 4
Utangulizi
Dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2000-2025, iko mbioni kutamatika. Na sasa mchakato wa kupata dira mpya ya maendeleo ya taifa ya miaka 25 yaani TANZANIA TUITAKAYO ya kuanzia 2025- 2050 unaendelea. Vipo vipaumbele ambavyo wanajamii tungetamani viwepo katika nyaja mbalimbali. Hapa nitazungumzia kuhusu kipaumbele cha maadili nikienda sambamba na nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu, yakutaka maadili iwe moja ya vipaumbele katika dira.
Agenda ya maadili ni suala mtambuka ambalo uhusisha watu wa rika tofauti, kutenda kwa ustawi wao na wajamii kwa ujumla. Chanzo cha maadili hua ni familia, ambapo mtoto ( ngazi ya kwanza ya ukuaji wa binadamu) huanza kujifunza kutoka kwa watu wa karibu yake, kwa kuiga (imitatation)mambo wanayofanya, mfano kujaribu kuvaa viatu vyake au vya watu wengine, kuita majina ya watu, kusalimia nk. Hivyo maendeleo ya tabia ya mtu huanza utotoni yakichochewa na malezi ya wazazi makuzi ya jamii inayomzunguka kuelekea ujana, na utu uzima. Hivyo jamii inahusika moja kwa moja kulaumiwa kwa mmomonyoko wa maadili. Mwana falsafa na mwandishi Jean Jacques Rousseau aliwahi kusema kwamba "all children are born pure but the society is a of evil"
Hali halisi ya mmomonyoko wa maadili Tanzania
Toka miaka ya 1990s na kuendelea 2000s kumeshuhudiwa na wimbi la mmonyoko wa maadili ambapo visa vingi vimeripotiwa. Ongezeko la talaka, ukatili kwa watoto, ubakaji ulawiti,ambapo jamii ya Tanzania imeshuhudia anguko la maadili kwa kuwepo tabia za ushoga, usagaji na uwepo wa vikundi vya uporaji vilivyojipa majina mfano panya road, kutoka dar es salaam.
Vipaumbele vya maadili kwenye dira ya 2050.
Ni ukweli usiopingika kwamba fursa yeyote hutengenezwa kutokana na changamoto zilizopo, hivyo basi ili kuondokana na janga hili na kuwa na Tanzania taifa lenye nguvu kiuchumi na ustawi wa jamii kwa vipaumbele yafuatayo.
Sheria ya kupeleka jeshini vijana walio nje ya mfumo wa elimu wa kawaida wenye umri wa kuanzia miaka 16hadi 20. Ili kujifunza uwajibikaji ,kujiamini, kujituma, kujitegemea uzalendo msimamo wa kutekeleza malengo ya kimaisha pasipo kuyumbishwa na tamaduni za
kigeni.
Ubunifu wa teknolojia katika kutengeneza mfumo wa kufunga kamera za usalama nyumbani na kuunganishwa na simu janja ya mzazi au mlezi
Kuanzishwa program ya michezo Shuleni na kuwapatia elimu ya jando na Unyago katika muktadha wa maadili mema kuanzia msingi. Kuwajenga watoto ufahamu kuhusu jinsia na haki na wajibu wao na kutambua viashiria vya unyanyasaji na aina zake.
Kuchukuliwa hatua Kali za kisheria wote wanaoweka mtandaoni maudhui yaliyo kinyume na desturi zetu, kwa kuwachapa viboko thelathini pindi waingoapo gerezani na siku watokapo na kuhakikisha kuwapatia kazi ngumu za kilimo na ujenzi ili washiriki katika uzalishaji mali.
Kurudishwa kwa somo la dini mmashuleni, kwa kuhakikisha kila mwanafunzi anahudhuria kipindi kulingana na dini yake.
Halmashauri kwa kushirikiana na serikali za mitaa na vijiji iwapatie kazi za kujitolea za kijamii kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 watoto wa majumbani, wanaoishi kwenye mazingira magumu na watoto wa vituoni. kuimarisha uwajibikaji kwa watoto na uzalendo, mfano program ya usafi wa mazingira sambamba na mafunzo ya maadili kushinda changamoto binafsi, kuzifahamu haki na wajibu wao.
Uwepo wa Sheria itakayowapatia vijana haki ya kuwa na nafasi za uwakilishi bungeni, na katika kamati za maendeleo kama ilivyo kwa wanawake na sio tu utashi wa kisiasa
Ili kuwapa vijana fursa ya kujifunza, kukutetea maslahi yao ndani bunge. Hivyo vijana wenyewe waione fursa ya kuchangia kutoa maoni katika mchakato wa dira ya maendeleo kwa njia ya simu na kujaza dodoso mtandaoni mfano wake hapo chini.
Chanzo ; c- The chanzo
Kuanzishwa kwa mabaraza ya maadili ngazi ya mtaa na Kijiji. Wadau mbalimbali hasa viongozi wa serikali ya mtaa, viongozi wa dini, wawakilishi wa makundi rika, afisa ustawi wa jamii, polisi jamii na wazee wa mila. Kwa lengo la kushauri kuonya kuchukua hatua stahiki dhidi ya viashiria vya unyanyasaji ngazi ya mtaa/Kijijji.
Kuanzishwa kwa chombo cha ufuatiliaji kwa mashirika yasiyo ya kiserikali,madhehebu ya dini na nyumba za malezi za watoto kujiridhisha utendaji kazi wake kwenda sambamba na maadili yetu kwa kulinda mila na desturi njema.
Kuwekeza kwa bima maalum ya mtoto chini ya mwamvuli wa NSSF, kwa njia ya simu Mzazi atalazimika kuweka akiba ya mtoto mara tu atakapozaliwa mpaka atakapotimiza umri wa miaka kumi na nane, kwa kuchangia kima cha chini cha shilingi 2000 kwa wiki, sawa na 8000 kwa mwezi na sh. 96000 kwa mwaka. Ili kuwezesha kijana kupata mtaji pindi aanzapo kujitegemea. NSSF watumie program ya simu kumuwezesha mzazi hata wa kijijini kuchangia kwa mitandao ya simu na kupata mrejesho wa uchangiaji, kupitia simu ya mkononi
Kuajiri maafisa ustawi wa jamii ngazi ya kata ili kurahisisha upatikanaji wa ushauri nasaha. Hasa kwa vijana wenye uraibu kupata ushauri na tiba.
Kuwapa wazazi fursa ya elimu ya malezi ya mtoto katika kliniki.
Serikali za mitaa na vijiji ihakikishe uwepo wa ulinzi na usalama kwa kufahamu idadi ya wakazi wanaohamia na kuondoka kwa kujiandikisha kwa wajumbe wa nyumba kumi, na kuimarisha polisi jamii. Kuzuia kuwepo kwa vikundi hatarishi vya vijana pasipo kuwa na sababu za msingi au shughuli ya maana.
Kuzuia unywaji wa pombe, uvutaji bangi na madawa ya kulevya.
Uwepo adhabu kali kwa watu wote wanayofanya ukatili wa kijinsia hasa ubakaji ulawiti na mauaji . Pia uwepo wa Sheria itakayo toza faini na adhabu kwa watu wote wasio waaminifu kwenye ndoa,(kuchepuka) hasa wale wanaotelekeza watoto bila kuwahudumia. Kuzalisha mabinti pasipo kuwaoa. Ni chanzo cha uwepo wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Kuwafilisi Mali na kifungo kwa wauzaji wa madawa ya kulevya.
Uwepo wa madawati ya kijinsia ngazi ya mtaa. Kwa kushirikiana na ofisi ya serikali za mitaa. Ili Kuboresha upatikanaji wa huduma na elimu ya jinsia kwa wana jamii ngazi ya mtaa,
Nafasi ya viongozi wa dini katika kulinda maadili.
Viongozi wa dini wana wajibu wakuhubiri upendo, hofu ya Mungu katika utendaji kwa waumini na kuhimiza, uaminifu kwenye ndoa, upendo. Na kukemea waziwazi vitendo vya ushoga na viashiria vyake, kwa kuwakumbusha wajibu waliopewa na Mungu katika kulea watoto watakao wapata kwenye ndoa, kuwalea kwa upendo na maadili ili kuwa na tunu ya ubinadamu.. Kuhakikisha kufahamiana kwa wanandoa watarajiwa. Kupanga uzazi yaani watoto watakaomudu kulea. Kua na vyanzo vya mapato imara.
Nafasi ya wazazi
Wazazi wanapaswa kurudi katika nafasi zao za asili.
Nafasi ya baba
Baba ni kichwa, kiongozi hivyo huwafundisha watoto hasa wakiume, kujituma, kuwajibika, kuwa mwaminifu, na walinzi wa familia
Nafasi ya mama
Muumbaji, ni muonaji huona hatma za watoto angali wadogo, pia huona janga kabla halijatokea
Wazazi wanapaswa
Kuwapenda, kuwatunza, kuwalinda, kutoa muda wa kuzungumza, kuwafundisha mafundisho ya dini, Imani na hofu ya Mungu, kupata elimu bora.
Hitimisho.
Mmomonyoko wa maadili hupelekea kwenye machafuko na uharibifu mwingi hivyo kila mmoja ana wajibika kulinda maadili kwa ajili ya Tanzania ya kesho.