Diamond Platnumz ajibu shutuma ya kudaiwa Wasafi ni wanyonyaji

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
15,236
21,225
Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz akifanyiwa mahojiano na kituo Cha habari cha DW Swahili nchini Germany amejibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mwanahabari Moja Kati ya swali ni kuhusu tuhuma ya baadhi ya watu kusema Wasafi ni wanyonyaji.

Diamond amejibu kama ifuatavyo

Nimekuwa nikiwachukua wasanii wachanga nakuwaleta Wasafi wakiwa hawana majina na kuwageuza kuwa biashara kwa kuwekeza hela nyingi unakuta natumia mpaka 500M Kwenye uwekezaji kwa msanii mmoja katika kubrand, kumtangaza na kufanya sanaa yake iwe kubwa ndio maana baada ya kumchukua msanii tunamfundisha vitu vingi Kwenye industry ya mziki ambayo alikuwa hajui tunamsaidia kwenye kuimba, kucheza na namna ya kumaintain status yake kwenye mziki ndio maana unakuta kabla ya kumtoa msanii inatuchukua miaka au miezi ili kumfanya awe full package kabla hatujamtambulisha kwenye industry.

Industry yetu inazidi kukua na baadhi ya mambo watu wanaanza kuyaelewa hasa yanahusu biashara ya mziki tunachofanya sisi Wasafi ndio hata industry ya mziki wa Marekani wanafanya kwenye label nyingi shida ni Moja msanii ukishamfanya kuwa mkubwa na akishaona hela nyingi zinaingia kwenye label anaingia tamaa anatamani hela yote angekuwa anapata yeye ndio maana anaona kama ananyonywa, anashindwa kujua hii ni biashara na tumewekeza hela nyingi kwake, hakuchangia chochote kipindi tunamkuuza.

So lazima kuwe na return ya kile tulichowekeza mfano mimi sio kwamba hela zote napata peke yangu, lazima niwalipe wakina Sallam, Babu tale na Mkubwa fella ndio biashara ilivyo hauwezi kuondoka kirahisi tu njoo hapa tumalizane wakati pia hii label inalipa kodi na ipo kisheria na inatambulika na mamlaka ya mapato mfano last year tumelipa kodi 100M hivi tukikuachia kirahisi tu nani atalipa kodi? Hivi kuhusu kipaji kingine tutachokileta kwenye label nani atagharamia?

Nini Maoni yako kwenye majibu haya ya Mondi
 
Kwahiyo Diamond anataka tuelewe kuwa Rayvan ameingia tamaa baada ya kuona mapato makubwa ya lebel akatamani hela zote ndiyo maana akajitoa?

Diamond amepanic hadi anatoa maneno yatakayosababisha hata Rayvan aanze kufunguka negative side mapema-mapema.
 
Alichoeleza Mondi ndio ukweli wenyewe, sasa wewe kama unaona ni panic utakuwa hupendi ukweli.
 
Huwa simpendi Diamond na vituko vyake, ila kwa hili yuko sahihi.

Wasafi ni music label, wako pale kutengeneza pesa kupitia muziki, sio kutoa msaada wa kukuza majina ya watu bure!

Kabla ya wasafi, Rayvanny alikuwa wapi? Harmonize alikuwa wapi? Vipi hapo walipofika leo, wangeweza kufika bila label ya Wasafi?

Hakuna kitu kinaitwa "Unyonyaji" kwenye dunia ya mabepari. Umepewa mkataba, ukausoma, na ukaona unafaa ukasaini. Hakuna la ziada hapo. Nitaamini Wasafi ni wanyonyaji siku akitokea mtu akatae mkataba wao mwanzoni kabisa kabla ya kupata umaarufu.

Sio mtu unatolewa Manzese huko, watu wanakubrand, wanakupambania unahit mpaka nje ya nchi, halafu wakichukua return ya uwekezaji wao unasema wanyonyaji. Hakuna free lunch dadek!
 
Kwahiyo Diamond anataka tuelewe kuwa Rayvan ameingia tamaa baada ya kuona mapato makubwa ya lebel akatamani hela zote ndiyo maana akajitoa?

Diamond amepanic hadi anatoa maneno yatakayosababisha hata Rayvan aanze kufunguka negative side mapema-mapema.
Ngoja nikueleweshe point yake ni hivi Lebo inakuchukua wewe unachangia mashairi na sauti wao wanachangia pesa ya kuwekeza kwako nk hivyo ni kama kampuni kunakua na hisa sasa ikitokea pesa imepatikana lazima kila mtu apate kutokana na hisa zake sasa baada ya muda wasanii wakiona hela nyingi wanapata tamaa ya kuchukua hela yote amesahau kama kuna watu wameweka hisa zao ndo maana akasema kama unataka hisa zote basi zinunue zote ili umiliki zote 100% kwa kuelewa zaidi kaisikilize DW.
 
Msanii wa kimataifa Diamond Platnumz akifanyiwa mahojiano na kituo Cha habari cha DW Swahili nchini Germany amejibu baadhi ya maswali aliyoulizwa na mwanahabari Moja Kati ya swali ni kuhusu tuhuma ya baadhi ya watu kusema Wasafi ni wanyonyaji.
Halafu haya mambo ya kuhisi unanyonywa wakati ulisaini mkataba ukakubali fungu lako kama ni bangi hivi tena walikuwa nayo wasanii wa zamani na ndio maana walishindwa kuendelea. Diamond amebaki kuwa na heshima kwa menejimenti nzima anavuna mbivu anapiga kazi.
 
Ngoja nikueleweshe point yake ni hivi Lebo inakuchukua wewe unachangia mashairi na sauti wao wanachangia pesa ya kuwekeza kwako nk hivyo ni kama kampuni kunakua na hisa sasa ikitokea pesa imepatikana lazima kila mtu apate kutokana na hisa zake sasa baada ya muda wasanii wakiona hela nyingi wanapata tamaa ya kuchukua hela yote amesahau kama kuna watu wameweka hisa zao...ndo maana akasema kama unataka hisa zote basi zinunue zote ili umiliki zote 100% kwa kuelewa zaidi kaisikilize DW.
Tena mashairi yenyewe unafindishwa namna ya kuandika, umekuja unaandika kama la saba B
 
Huwa simpendi Diamond na vituko vyake, ila kwa hili yuko sahihi.

Wasafi ni music label, wako pale kutengeneza pesa kupitia muziki, sio kutoa msaada wa kukuza majina ya watu bure!

Kabla ya wasafi, Rayvanny alikua wapi? Harmonize alikua wapi? Vipi hapo walipofika leo, wangeweza kufika bila label ya Wasafi?

Hakuna kitu kinaitwa "Unyonyaji" kwenye dunia ya mabepari. Umepewa mkataba, ukausoma, na ukaona unafaa ukasaini. Hakuna la ziada hapo. Nitaamini Wasafi ni wanyonyaji siku akitokea mtu akatae mkataba wao mwanzoni kabisa kabla ya kupata umaarufu.

Sio mtu unatolewa manzese huko, watu wanakubrand, wanakupambania unahit mpaka nje ya nchi, alafu wakichukua return ya uwekezaji wao unasema wanyonyaji. Hakuna free lunch dadek!
Kiuhalisia mtu akiwa hana ramani hukubali lolote lile imradi aingie.
Akishaona amefanikiwa huanza mambo yake

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom