Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,735
- 14,095
Habari zenu wana JF wenzangu.
Katika pitapita zangu maeneo fulan nimekutana na hii habari kutoka kwa mtu wa karibu mno wa msanii huyo, akidai kwamba Diamond yuko katika mchakato wa kulishangaza taifa hapo mwakani.
Japo mimi sio mwanasiasa, lakini ningependa kumshauri ndugu yetu Diamond afikirie mara mbili uamuzi wake huo. Asije kuingia huko kichwa kichwa akaanza kufanywa mtaji wa kisiasa na hawa wanasiasa wetu uchwara wanaofanya siasa zao kupitia mgongo wa majina ya watu maarufu nk.
Na kama kweli ana lengo la kushinda uchaguzi basi akagombee katika jimbo moja la kwao Kigoma, maana kule anakubalika kuliko yule mmanyema mwenzake kwa jina anaitwa Zito.
Wewe kama mwana JF, una nini la kumwambia ndugu yetu Dangote wa Tandale.
Lisemwalo lipo, na kama halipo laja.