BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,810
Baada ya Harmonize kutoka hadharani na kutamba kwamba, hataongea na Msanii yeyote wa Afrika Mashariki ambaye hamiliki gari aina ya Range Rover! Leo Diamond Platnumz ni kama amerusha kijembe kwa Kondeboy kupitia insta story yake.
Chibu ameweka video ya Zuchu ambaye amejinunulia gari aina ya Range Rover na kisha kuandika kwamba, gari hizo rasmi ni kwa ajili ya Wanawake!
Ameandika; “Unajua kunifanya nitembee kifua mbele Zuuh. Naomba Kuanzia leo Nirasimishe rasmi kwamba Range ni gari Maalum kwajili ya Queens wote wapambanaji Mjini wakiongozwa na @officialzuchu “ - ameandika Diamond.