Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,061
- 1,637
Kurushwa na umeme ni dhana hakuna kitu kama hicho kisayansi ,ukweli ni huu hapa.
Kuna kauli umesha wahi zisikia,mtu akisema amerushwa na umeme si ndiyo..??
Mtu huyo anaweza shuhudia kabisa kuwa karushwa na umeme toka sebuleni hadi chumbani...
Basi ukweli ni huu,umeme haurushi mtu,ila umeme unaweza
1. Shika mtu na akashindwa kujitoa.
kama tu huo umeme utakua katika kiasi cha kupoozesha mfumo wake wa fahamu...mtu huyo hata jichomoa ataganda hapo hapo hadi maji yake mwilini yapungue ndo ataachiwa...
DHANA YA KURUSHWA NA UMEME.
2. Ukikuta umehisi umerushwa na umeme maana yake umeme uliingilia mifumo yako ya fahamu na ukashindwa kukushika(kukunasa,kulukausha maji),hali iliosababisha wewe kupata hitirafu ya fahamu,ya kumbukumbu ambapo ulihama mwenyewe eneo moja kwenda jingine bila kujitambua...
Fahamu kua mfumo wa fahamu wa binadamu huwasiliana kwa njia ya umeme..na ikitokea umeme wa ziada umeingia katika mwili hupelekea mfumo huo kuvurugika...
Pale binadamu anapogusa umeme bahati mbaya,ubongo wake husababisha awashe hisia za kujiokoa..
Kwakua kilichosababisha changamoto ni umeme husababisha taarifa mvurugano hupelekea mtu huyo kusahau nyakati flani ambazo alikua akijiokoa..
Hivyo kama ikitokea umegusa kifaa cha umeme sebuleni na baadae ghafla ukajikuta chumbani si kwamba umerushwa hadi huko...hapana
Ulikimbilia huko wewe mwenyewe kwa miguu yako...sema tukio lilitokea kwa haraka ukiwa katika hali ya kupoteza kumbukumbu...kutokana na mfumo wako wa fahamu kuingiliwa na umeme...
So pale kumbukumbu zitakapo kurejea utahisi umefika hapo kwa kurushwa...
Kuna mmoja alirushwa toka jikoni hadi kwa jirani....hahahah
USIKU MWEMA.
Transistor.