Dhana ya kuchoma moto tunguli

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
282,475
734,779


Ni kiini macho na aina fulani hivi ya utapeli..kwamba eti mchawi ajisalimishe na kukabidhi mikoba yake yenye matunguli ya kila aina, huyo hawezi kuwa na maisha tena! Asipouliwa na wenzake atakufa mwenyewe

Uchawi ni fani inayojitegemea yenye kanuni taratibu na masharti yake tena magumu, ndio maana si wengi wanaweza kuwa wachawi! Uchawi una mahusiano ya moja kwa moja na ulimwengu wa giza na mambo yasiyoonekana ulimwengu wa roho kuna viapo vyake huko! Tunguli na mapembe ni vibebeo tu vya nguvu isiyoonekana ni catalysts, kwahiyo mchawi wa kweli ana uwezo wa kuihamisha nguvu husika na kuacha mitunguli mitupu isiyo na nguvu yoyote kama mikasha tuu

Mchawi wa kweli hawindiki na wale wanaojifanya kutoa wachawi, mkikaribia nyumba yake msipokutana na bahari basi mtakutana na msitu au kiwanja kitupu... ..na huyo anayefanya hiyo kazi ni lazima awe amejizatiti kwa kinga za kila aina na zenye nguvu kubwa sana

Hii ni kwakuwa uchawi una wataalam na madaraja yake . kwahiyo kama daraja langu ni dogo na nikiona kuna mapambano yanakuja haraka sana hutafuta msaada kwa aliye juu yangu au aliyenifundisha kazi...lakini hapo hapo pia naweza kuwa ninamiliki silaha zangu za kinga za maangamizi kwa yeyote yule atakayejaribu kunichezea!

Hawa kina manyaunyau walikuwa ni matapeli na wapigaji tu wakikamata matapeli na wapigaji wenzao wanaojua mazingaombwe na kujifanya ni wachawi ama waganga mahiri wa kienyeji. Kundi lingine la kitapeli ni hili la manabii na mitume wa kileo ambao wamegeuza vitu vyao kama kliniki za washirikina kwa kutumia jina la Yesu Kristo

Tunguli halisi haiungui kwa moto wa kawaida..upo moto wa kichawi ambao ndio unaweza kufanya hiyo kazi au moto wenye nguvu ya kimungu na ni aina ya moto ambao hauunguzi kingine chochote zaidi ya kilichodhamiriwa
Wale wabebao matunguli na kuyapeleka kanisani kuombewa kisha kuchomwa moto wanakuwa tayari(hata kama ni wakweli)hawana nguvu tena na walishafukuzwa kilingeni na kupokonywa nguvu zote.

Ni wachache mno wanaoamua kutoka wenyewe tena kwa kutoroka na kwenda kupata ulinzi wa Kimungu kabla wenzao hawajawastukia kwwakijua





Hizi operations nyingi vijijini za kutoa wachawi ni ujinga tu wa jamii yetu na kutoelimishwa dhana nzima ya uchawi na jinsi unavyofanya kazi
Kanda ya ziwa Kumekuwa na mauaji mengi ya kutisha ya vikongwe wakihisiwa ni wachawi....ujinga mkubwa huu!!! Tuache maskhara mchawi wa kweli hukuona na kukuwahi kabla hujamfikia

Jinsi tunavyozidi kulipuuzia suala zima la uchawi na ushirikina ndio jinsi tunavyozidi kuiumiza jamii
Wenzetu ulaya wanafundisha uchawi kama somo hii imesaidia kuepusha matatizo mengi sana...tusifungwe na nira za kiimani na kuonekana kuzungumzia uchawi na ushirikina ni jambo baya sana..tunapotoka na kukosea sana...kwakuwa hata katika hizo imani zetu zinaukubali na kuukiri uchawi kama nguvu hasi inayofanya kazi duniani juu hufiki popote
 



Ni kweli mkuu kuhusu hawa manabii wa kinigeria na wa hapa bongo. Nashindwa kuelewa mtu unakuwa na akili gani mpaka unarubuniwa akili na fake pastors. Kwa kweli binadamu yabidi Tumuombee Mungu atuangazie mwanga.
 
Ni kweli mkuu kuhusu hawa manabii wa kinigeria na wa hapa bongo. Nashindwa kuelewa mtu unakuwa na akili gani mpaka unarubuniwa akili na fake pastors. Kwa kweli binadamu yabidi Tumuombee Mungu atuangazie mwanga.
Haya mambo huwezi kuta ulaya kwasasa kwakuwa walishayapitia na kuona athari zake kwahiyo wakaamua kuutafiti na kuufanya uchawi kama somo rasmi...serikali zao zikasaidia hata ujenzi wa shule na vyuo...jamii zao kwasasa zimeelimika
 
Nnachokumbuka mimi kabla ya kushamiri kwa haya makanisa ya kilokole miaka ya mwanzoni ya 90 kanisa Katoliki halikuwa na mafundisho ya mambo ya mapepo, mara uchawi au eti mtu katenda dhambi kwa kuvunja amri za Mungu anaambiwa ana mapepo mf pepo la ngono. Hapa dhambi imegeuka pepo kuwa aliyetenda dhambi hana hatia coz wachawi wamemrushia pepo la ngono au la wizi nk. Ikawa walokole wanaamini mtu akiugua sio kawaida ni pepo wataomba wakiona hamna matokeo mazuri wanakimbiza hospitali ikiwa bahati yake anapona akiwa amechelewa sana ndo mnamkosa huyo. Kwa kweli itachukua mda sana watu kubadilisha imani hii kwa ajili ya matatizo mbalimbali ya maisha ambayo yanafanya watu waishi kwa hofu kubwa. Ndoa/ mahusiano/ mapenzi, ajira/ uchumi/ elimu/ madaraka/ kipato, familiia/ watoto/ ndugu nk nk nk. Wajanja wataendelea kuwaliza wajinga.
 
Mkuu umetoa elimu nzuri sana kwa watanzania, tatizo kubwa linalotukabili watanzania ni elimu ndiyo maana tunafikiri utajiri unapatikana kwa kutumia viungo vya albino(zeruzeru)
 

Ila usisahau na wale walioanzia hospitali, wakashindikanwa baadaye wakapelekwa kanisani wakapona.
 


Mkuu, nilitamani sana ungeongelea ukuu wa Nguvu za Mungu kwa kuwa kwa fani yako lazima utakuwa unaifahamu ila sijui kwa nini huiongelei kwa sana. Shetani anaposhindwa, Mungu anaweza. Kama wachawi kwa jina la uganga hawawezi bado uko sahihi kwa kuwa hata Biblia imeandika Shetani hawezi kumtoa shetani mwenzake. Vinginvyo ufalme wake umefitinika.

Ongealea nguvu ya Mungu inavyoharibu uchawi na nguvu za shetani maana hiyo ndiyo kazi ya Yesu kuja duniani. Kuzivunja kazi za ibilisi.

Kuna wengine akili zao hapa zimeishia katoliki. WAnaona eti nguvu ya Mungu lazima ipatikane katoliki na kwa kuwa katoliki hawana basi hakuna tena hiyo nguvu. Ujinga wa kiroho. Msingi wa Wakristo ni Neno la Mungu na wala si madhehebu.

Waambie watu ukuu wa Mungu katika kuzivunja kazi za adui na uache kuwachanganya kwa kuwaambia habari za dini, madhehebu na mambo ya watu binafis.

Wapo watu wanaojihukumu kwa kushindwa kwao au kukosa kumjua Mungu na hivyo kuwa na wivu kwa kilakitu kinachomthibitisha Mungu. Na hivyo utawaona wako tayari kushabikia kwa amani kabisa nguvu za uchawi na uganga ambazo ni cha mtoto sana kwa Mungu, kisha wakaandia Imani ya Mungu kwa sababu hawamjui Mungu ila wanazo dini tu.

Kuna mwingine kase,a eti katoliki halikuwaga na neno mapepo (Huu ni upumbavu) kwa sababu laiti kama angelikuwa anasoma neno la Mungu angetambua kuwa Mapepo yameandikwa hata kwenye Agano la Kale miaka mingi tu kabla ya huo ukatoliki kutengenezwa na watawala (baada ya Kristo).

Ninatamani pia usiishie kusisitiza kukandia manabii as if Mungu hawezi kuwa na manabii. Biblia imesema wapo na watakuwepo. Ninatamani sana ungeanisha kati ya manabii wa uwongo na watumishi wa Mungu badala ya kuishia kusema kinyume cha manabii as if una vita nao. Biblia imesema wazi sana kwamba "Hata shetani hujigeuza na kujifanya kama malaika wa Nuru", hivyo si ajabu kweli pepo kujifanya li wakala la Mungu, lakini haina maana kwamba shetani kameza malaika wote wa Nuru ana kwamba sasa Mungu hana malaika tena". Biblia imeandka Bwana Yesu aliwaonya wafuasi wake (siyo waumini wa kanisa katliki kwa kuwa hiyo katoliki haikuwepo wakati wa yesu kama wengine wanavyodanganywa), aliwaonya wanafunzi wake, yaani wafuasi wa Kristo kwamba "Angalieni mtu asiwandanganye, kwa maana wengi watakuja kwa jina langu wakisema Mimi ni Kristo". Hapa ni kweli Yesu alijua wengi watakuja katika siku za mwisho kwa jina la kumkiri Yesu kwamba ni Kristo, lakini ni kwa udanganyifu, hakuishia hapo tu tena akaonya kwamba msiiamini kila roho bali zichunguzeni kama zatokana na Mungu".

Lakini hakuwa na maana kwamba Hapatukuwa na WAtumishi wa Mungu alilye hai, hakumaanisha kwamba Roho zitokanazo na Mungu hazitakuwepo tena, wala hakumannisha kwamba WAtumishi wa Mungu, we kweli hawatakuwepo tena kama wengine wanavyoshadadia na kwa ujinga wa kutokulijua neno, hata wanadiriki kusema kwamba "Makanisa ya Kipentekoste ndiyo aliyokuwa anayasema Yesu", wakasahau kwamba andiko limenena "Sitawaacha Yatima, bali nitawaletea Roho Mtakatifu atakayewafundisha kweli yote". Tena "Ziko karama, na huduma mbali mbali katika kanisa la Mungu lakini Azitendaye ni Roho Yeye Yule ambaye humgawia mtu kama vile yeye apendavyo.

Wengine, mitume, Wengine aina za Lugha, wengine Manabii, Wengine Walimu, Wengine karama za kuponya, Wengine, Kuonya, Wengine Wainjilisiti, Wengine matendo ya miujiza, n.k n.k. Biblia imeendelea kusema "Vitu vyote vitakoma lakini maneno yangu hayatapita kamwe".

Anayesema kwamba kwa sasa hakuna watumishi wa Mungu alete maandiko tujadili ambapo Neno limesema siku za Mwisho duniani watumishi wa kwlei wa Mungu hawatakuwepo ila watajaa Masela wasanii.

Ninawaonya wanaosimamia katika dni kwa uzamani wake kwa sababu hadi Yesu anatwaliwa hakuna dini aliyokuwa ameiunda. Kwa nini usianze kutafiti maandiko uone uanzishwaji wa hiyo dini yako ya zamani iliundwaje ili utambue kama si moja ya vikundi ambavyo Yesu alivitolea tahadhari? Hasa ikiwa imani hizo zinaendeshwa bila watu kufindishwa Biblia wala kusoma, ila kujikita katika mapokeo tu?

Mshana Jr. Nitafurahi sana, ukiwa unajikita kuwaambia zaidi Ukuu na Uweza wa Nguvu za Mungu na kwamba Zipo Zinafanya kazi na hazifungamani na madhehebu ama kanuni za kimapokeo ya vikundi vy akibinadamu ila Zimeasisiwa na kusimikwa katika Maandiko. Na kwamba Wapo watumishi wa Mungu ambao Mungu anawatumia na Mungu haheshimu dini na madhehebu ya Watu bali huliangalia Neno apate kulitimiza.

Mchana mwema kiongozi.
 
Noted Tabby with so much appreciations, nimekuelewa vizuri nitafanya hivyo sooner or later
 
Noted Tabby with so much appreciations, nimekuelewa vizuri nitafanya hivyo sooner or later

Ambiere u muandishi mzuri sana lakini unaandika vitu ambavyo vina negative perception withn our society ,sometime wengine tunaogopa hata kusoma what if u change ur vision na kutumia kipawa hicho kuandika juu ya Mungu wetu na kuokoa kizazi cha tulio misri
 
Noted
 
Kanisani hakuna dawa. Mtu akiugua ni lazima kuna source ambayo mara nyingi ni virus au bacteria. Huwezi kupiga prayer na kuombea mapepo ili mtu huyu apone na akapona. Kuna maradhi ya kiimani yatokanayo na fikra au ya kutupiwa na wachawi kupitia majini n.k Haya ni rahisi kuyatoa kwa maombi maalum eidha ya kiislam au ya kikristu na Wala sio mijiza kama wanaoona wanaamini kisha wanakuwa watumwa wa imani hiyo.
 
Haya mambo huwezi kuta ulaya kwasasa kwakuwa walishayapitia na kuona athari zake kwahiyo wakaamua kuutafiti na kuufanya uchawi kama somo rasmi...serikali zao zikasaidia hata ujenzi wa shule na vyuo...jamii zao kwasasa zimeelimika
Tuwekee mfano wa hvyo vyuo
 
Umesema hao wanaochomA zana zao wameishiwa nguvu??hzo nguvu zimemalizwa na hao unaowaita manabii feki wakati wapo watu wa mungu wasiojiita vyeo vyovyote wanachoma moto tunguli kweli kweli.
 
Umesema hao wanaochomA zana zao wameishiwa nguvu??hzo nguvu zimemalizwa na hao unaowaita manabii feki wakati wapo watu wa mungu wasiojiita vyeo vyovyote wanachoma moto tunguli kweli kweli.
Iko hivi tunguli ni makapi tuu inapofikia hatua ya kuzichoma, kama umenisoma vema ni kwamba kuna tunguli hazichomeki na pia kuna uchawi hautumiii kabisa tunguli kwa mfano uchawi wa majini na mizimu
 
Ila usisahau na wale walioanzia hospitali, wakashindikanwa baadaye wakapelekwa kanisani wakapona.

Usanii tu,wachungaji na manabii wengi wasanii tu,km wanawaombea wagonjwa wanapona,sasa siwaende ma hospitalini kuwaombea wapone, upuuzi mtupu,,,,,,,,ukiumwa muombe mungu mwenyewe utapona km ugonjwa ni wa sihili,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…