Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,668
- 119,281
Wanabodi
This is a developing story
Yaani story muendelezo
Jana jioni katika eneo la Magomeni Usalama, Gari Toyota Landcruiser Hard Top No. DFP 8106 Yagonga mtu na kumua kwa ajali, mwanamke mmoja. Mwanzo gari na dereva wake walidakwa na kuhifadhiwa kituo cha polisi cha Magomeni Polisi. Leo Dereva Amesepa, kwa kusepeshwa na Polisi!
Itaendelea kesho.
Paskali
Update 1.
Update 1.
P.
This is a developing story
Yaani story muendelezo
Jana jioni katika eneo la Magomeni Usalama, Gari Toyota Landcruiser Hard Top No. DFP 8106 Yagonga mtu na kumua kwa ajali, mwanamke mmoja. Mwanzo gari na dereva wake walidakwa na kuhifadhiwa kituo cha polisi cha Magomeni Polisi. Leo Dereva Amesepa, kwa kusepeshwa na Polisi!
Itaendelea kesho.
Paskali
Update 1.
Update 1.
- Jina la Marehemu ni Anastazia Benedict, mwenyeji wa Kigoma, ni single mother wa watoto wawili, ni mfanyabiashara wa biashara ndogo ndogo soko la Magomeni.
- Hiyo Gari, DFP 8107 ni gari ya taasisi fulani nyeti ya serikali, nilipoisaka kwenye mtandao wa bima , gari hiyo haina bima, hivyo sasa ni taasisi husika ndio itahusika kumfidia marehemu.
- Ajali ilivyotoke: Anna alikuwa anavuka barabara kwenye zebra, pale kituo cha mwendokasi cha Usalama, baada tuu ya basi la mwendokasi kutokea Marogoro Rd, kwenda mjini, yeye akavuka mbio. Kumbe dereva wa DFP alikuwa anakuja kwa kasi upande wa no entry kuelekea Ubungo!, ikamgonga mazima, na dereva hakusimama, akasepa moto na moto wake. yaani kafanya "hit and run"
- Madereva wa bodo boda wa hapo usalama, wakaamua kulala nae, kwa kumfuata kwa nyuma, mbele kidogo kukawa na basi la mwendokasi linakuja, hivyo akiendelea watagongana uso kwa uso!. Dereva akalipandisha kari kwenye tuta la mwendokasi, gari likagota!.
- Akafungua mlango na kusepa kwa kukimbia kwa miguu, akakimbilia kanisa la Baptist, ili kujiokoa asiuawawe na wananchi wenye hasira!. Boda boda shujaa wale, wakaacha boda boda zao na kukimbia nae mpaka hapo kanisani. Wakasema hawatoki mpaka watoke na mtuhumiwa wao wamalizane nae kama yeye alivyomalizana na yule aliyemgonga. Kanisa likampa hifadhi huyo dereva, boda boda wakawambiwa hatolewi hadi waje na polisi.
- Kule barabarani, wasamaria wema wakauchukua mwili ukiwa bado hai, wakauwahisha Magomeni hospital, wakatakiwa wakachukue PF3 Polisi kuthibitisha ni ajali, wakarudi kituo cha Magomeni polisi , wakapewa PF3, wakarejea Magomeni Hospitali, wakaelezwa mambo sii mambo, wajibebee mwili wa mtu wao na kuupeleka Mwananyama hospitali. Kama yule dereva asingekimbia, angesimama na kutoa msaada, labda wangeokoa maisha ya huyu dada.
- Polisi wakafika kupima na kulichukua gari, vijana boda boda wakaelekeza mtuhumiwa alipojificha, polisi wakamdakua na kwenda nae kituoni Magomeni.
- Usiku mzima kulikuwa na heka heka hapo Magomeni Polisi magari ya DFP yakiandamana, kuingia na kutoka. Kufika leo asubuhi, ndugu walipofuatilia, ndipo wakaelezwa ni gari tuu ndio imepatikana, dereva hakupatikana, amesepa jumla!. Vijana wa boda boda wanasema ni polisi MigoMigo wamekula mingo ya kumsepesha!.
- Ndugu wakaja juu, haiwezekani jana dereva aletwe, halafu leo asubuhi waambiwe hajapatikana!. Wameelekezwa kama wana malalamiko yoyote wayapeleke kwa Afande RTO, pale Oysterbay polisi.
- Ndugu wamachotaka ni msaada tuu wa mazishi kumhifadhi ndugu yao mengine tutajua mbele ya safari.
P.