Sikiliza Live wanazungumzia Hali ya Njaa nchini Charles Tizeba amekana uwepo wa Njaa. Tundu Lissu amemkalia Kooni.
===========
WAZIRI TIZEBA
Amesema wabunge wanaolalamika leo ndio walioongea bungeni chakula cha ziada kiuzwe nje na tani milioni 1.5 ziliuzwa kwa utaratibu maalum katika ziada ya milioni 3.2.
Amesema ni upotoshaji kusema waziri mkuu amesema kuna tani milioni 1.5 zimerundikwa mahali bali zapo mikononi kwa wakulima
Amesema habari hiyo ina lengo la kutengeneza panic lakini hakuna soko ambalo halina chakula, kilichopo ni bei ya mahindi kupanda na imesababishwa na mahitaji makubwa kutoka nje na kupandisha bei za ndani
=> Swala la bei bei kupanda, demand ya mahindi ya Tanzania ni kubwa sana kutoka nje. Watu kutoka nje wanatoa bei kubwa kutokana na kwao kupata ukame na bei ya mahindi ilikuwa kilio na wabunge hawahawa na kuna maeneo huwa yana upungufu wa chakula miaka yote lakini kusema Tanzania ina njaa ni siasa za hovyo kwa sababu zinaleta panic sehemu ambayo haikupaswa kuwepo.
Labda mtu ambaye hajawahi kulima ndio hawezi kujua, ukame wa sasa hauwezi kuonyesha athari sasa bali zitaonekana baadae, akiba inaweza kupungua kuanzia mwezi wa nne/tano kama matokeo ya kulima hayatakuwa mazuri.
Ni kweli mahindi yetu yamepungua kwenye baadhi ya maeneo lakini mchele uko mwingi sana Tanzania mpaka hakuna mahali ya kuuza. Watu waachane na mazoea na kuendana na mazingira na hali ya hewa.
mkafrend
Kumekuwepo na mjadala mkali kati ya Waziri wa Kilimo Mhe. Charles TIZEBA, Mbunge wa Singida Kaskazini Mhe. Tundu LISSU, Mama mmoja wa MOROGORO na mchambuzi toka Kenya.
Katika mijadala hiyo Charles TIZEBA amesema nchi haina njaa kwa kuwa bado maeneo mengi maghala yana nafaka ya kutosha sambamba na masoko mengi nchini. Vile vile amekiri kuwa kilichopo nchini ni bei za vyakula kupanda lkn pia amelaumu Wabunge kwa kupitisha azimio la kuuza chakula nje hapo awali.
Sasa tujiulize:-
1. Charles TIZEBA aliporuhusu ktk ziara yake chakula cha NFRA kipelekwe Kagera ilikuwa kwa ajili gani - kusaidia watu wenye chakula au wenye uhaba wa chakula??
2. Hivi nchi kukabiliwa na njaa kwa wananchi wake huwa masoko hayana kabisa nafaka?? -
3. Nimesikia viongozi wa madhehebu ya dini Tanga kwenye YouTube wakisema njaa ipo lkn pia nimesikia kuwa Mkuu wa Wilaya Gondwe alitoa machozi kuona kaya zinazoishi kwa kula maembe - Je, huu ni uongo dhidi ya serikali ya magufuli???
4. Serikali inadhani inajibu maswali ya kaya, vijiji, wilaya na mikoa michache au mingi yenye kukabiliwa na upungufu wa chakula uliosababishwa na ukame???
5. Hoja yenye mwelekeo wa kulaumu wananchi na Wabunge kwa kuuza chakula nje ya nchi inayotolewa na Mhe. Charles TIZEBA ina mshiko. Ninavyofahamu mimi mkulima kuuza nafaka na mazao yake kwa bei shindanishi humpa zaidi mkulima faida kwa kuwa kadrii apatavyo fedha ndivyo huweza kutatua mahitaji muhimu kama kugharamia elimu, afya, umeme, mavazi nk nk
Hivyo si busara sana kwa MHE. TIZEBA kuelekeza lawama kwa watu hawa kuhusu uuzaji mazao.
6. Kama mvua zitanyesha hebu kwa pamoja tulime au kihimiza mkulima alime mazao yaivayo haraka