Deo Sanga aomba Rais Magufuli aongezewe muda hata asipotaka

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,178

Mbunge wa Makambako, Deo Sanga amesema Rais Magufuli amefanya kazi kubwa katika nafasi yake ya Urais.

Ametoa ombi la kuongezewa muda wa kubaki madarakani kama Rais ili mipango anayoendelea nayo aweze kuikamilisha.

Ameomba aongezewe muda hata kama asipotaka. Amesema hata China waliwahi kufanya hivyo kipindi fulani katika historia.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - CCM Zanzibar wapendekeza Rais Mwinyi atawale kwa miaka 7, wasema kufanya uchaguzi 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za umma

- Ally Kessy: Katiba sio msaafu, Rais Magufuli akimaliza muda wake tutatengua Katiba aongezewe muda | Spika Ndugai amuunga mkono

- Mzee Mwinyi: Rais Magufuli aongezewe muda wa miaka 5 zaidi kama shukrani

- Zile kelele za Rais Magufuli aongezewe muda mbona hazipingwi kwa Rais Samia?

- Uchaguzi 2020 - Dkt. Magufuli aongezewe muda wa kutawala

- Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala
 
"Rais wetu Dkt. Magufuli amefanya kazi kubwa, ombi langu hapa ndani atake asitake tumuongezee muda ili aweze kufanya kazi yake vizuri ili mipango aliyoipanga ikamilike, nilisema kipindi fulani hata China walifanya hivyo si dhambi kumuongezea anayefanya vizuri" - Deo Sanga

#Bungeni

IMG_0186.jpg


Kumekucha sasa lile bunge la kijani linaanza kazi waliyoipigania.
 
Nashangaa kumlamba ngede mwanaume mwenzako ili ule ni aibu as a man having both brain and arm muscles you shouldn't do it.

Ina mana kwani Huyo ndo akili kuliko Taifa zima. Let us assume akitokea akachukuliwa na aliyemleta duniani do you think kuwa life halitaendelea kweli kwa Watanzania.

Ila ccm INA mwisho wake.
 
Jiwe kapora kura za wapinzani na ndani ya ccm aliwakata wabunge wenye akili (mfano akina Adadi Rajabu, Andrew Chenge, Maganga Ngeleja, n.k) akapitisha wenye mtindio wa ubongo ili wapitishe maazimio ya kumbakisha madarakani.

Kwahiyo huu ujinga tulisha ufahamu tangu wakati wa mchakato wa kukata majina ya wagombea na kupora kura za wapinzani.
 
Haya mazee ya Darasa la 7 ndiyo hayajitambui kabusa. Na ndiyo yamejaa kwenye bunge hili. Full kujipendekeza ili kuficha madhambi yao kwenye biashara zao.

Namhakikishia Deo Sanga maarufu Kama Jah People kuwa MUNGU wetu aliye hai ATAINGILIA KATI kudhibiti hizo mbinu zenu za kumfanya Meko awe Rais wa milele.

Kuna kitu kitatokea kabla ya 2023, sisi tupige magoti tuzidi kuomba.
 
Back
Top Bottom