Demu wangu wa zamani ananishauri nioe beki 3 wake

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,423
55,258
WanaJF naombeni ushauri.
Baada ya kutendwa na demu niliyempenda sana nilkata shauri kuwa nile ujana mpk kieleweke. Ktk kula ujana huko palitokea wadada wenye nia ya dhati kabisa ya kuolewa na mm lkn niliishia kuwamega tu na kuwaacha solemba.

Mmoja wa wadada hao alinipenda sana, alionyesha mapenzi ya dhati kwangu na kunipa vya uvunguni kuliko maelezo. Nami kwa kuwa sikuwa tayari kuoa nilimzungusha mpk akakata tamaa.

Sasa hv kidume umri umeenda, nahitaji mke. Mwezi wa pili mwaka huu kunako fb huyo dada aliyekata tamaa (hatukuwa na mawasiliano kwa miaka 2) akanitaarifu ya kwamba yeye ameolewa na ana mtoto wa miezi 9.

Akaniuliza unaoa lini? Nikamwambia bado sijampata mtu sahihi. Nikimpata hata kesho naoa. nikamtania ya kwamba kama kuna mdada anayemfahamu katulia na ana tabia nzuri aniunganishe naye.

Baada ya wiki 2 kupita dada kanirukia hewani, haloo! Na akanijulisha kuwa mchumba kapatikana. Nikamwambia nipe jina lake analotumia fb/instagram ili nione picha zake. Nikatumiwa jina na kuanza kucheki. Mtoto yuko vizuri mno. Kidume nikavutika. Nikampa mrejesho ex-gf wangu kuwa kitu nakihitaji.

Mengi yaliendelea na mwisho wa siku nikakutana na binti mhusika. Huku na huku nikammega yule binti wa miaka 24. Kidume nikakolea nikajiapiza kuweka ndani mzigo.

Kumbe kwa muda wote huu binti alinidanganya mambo 3.
+Moja elimu yake, alidai amemaliza f4 kumbe ni la 7.
+Mbili mahala anapoishi, alisema anakaa kwa shangaziye kumbe anaishi kwa ex-gf wangu.
+Tatu kazi anayoifanya. Alisema anafanya kazi mgahawani kumbe beki 3.

Nimeyabaini haya baada ya kutaka kumtembelea ex gf wangu ili kumshukuru kwa kuniunganisha na king'asti huyu mwenye utamu wa halua. Akaona ataumbuka akaamua kuweka mambo hadharani.

Kuwa yule binti ni beki 3 wake na anakaa naye anamlelea mwanaye. Ufuuuu!!! Kidume nimepatwa na mshangao. Najiuliza niuache utamu huu uende zake ama niendelee na mipango ya kumuoa. Huyu ex gf hatonichafulia sifa yangu siku za usoni kuwa nimeoa beki tatu wake? Na je ni sahihi kwangu mm na masters yangu kuoa la saba? Kutakuwa na athari zipi ktk hili?

Nipeni mawazo ya kujenga ktk hili.
 
Haki tena,hizi "masters" ni bora sifa ya uwaziri na ukuu wa mkoa ibakie kujua kusoma na kuandika tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…