Demokrasia ndani ya CHADEMA inafutika polepole

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ilianza kwenye kuchagua mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA.

Kwa sasa hata kuchagua Katibu Mkuu imekuwa vivyo hivyo.

Wanachama wanaombwa wanyoshe mikono juu badala ya kupewa kalamu na karatasi ili watumie haki yao ya msingi kikatiba kuchagua kiongozi wanayemtaka ndani ya sanduku la kura za siri.

Hii dhana ya uoga ni dalili inayoonyesha kinachofanyika viongozi wanafahamu hakikubaliki na wengi!

Hii aina ya demokrasia imeanza kustawi ndani ya CHADEMA baada ya ujio wa Lowassa na genge lake.

Unawaambia wanachama wanyoshe mikono juu wakati umewaangalia usoni kwa kutumia sura ya kutisha.

Kilichofanyika ni sawa na making important decisions under duress na hii katika macho ya sheria ni void.

Chama cha Demokrasia lakini hakiishi katika demokrasia ya kweli.

Wanachama wanajengewa nidhamu ya uoga na kulea matatizo kwa sababu ukipingana kimtazamo na kihoja na maamuzi ya viongozi wakuu (wenye chama) unavalishwa jina la usaliti au umenunuliwa.
 
democrasi ipo ktk uongoz wa nchi hii umeya jiji la dar urais kule visiwan na hata hapa bara kukamata wapinzani nafikir democrasia hapo imekuwa kwa kasi wapongezeni wenyeviti wa ccm bado mpo kimya hamtak kuwapongeza kwa kuimarisha democracy bas ya chadema inakufa polepole tuwazomeeee chadema tuwapongeze ccm.
 
Daaah kaka kwa hiyo wewe katika Mkutano wote umeona cha kunyoosha Mikono tu?Vipi Katibu Mkuu unamuonaje?
 
"mbere, post: 15556424, member: 277324"]Kwani mkuu mbona ndugai na genge lake wanafanya hivyo bungeni na mambo ya kitaifa yanapitishwa? Au ccm ni kuku na chadema ni bata yeye huwa anaarisha tu Wakati wote?"

Asante kwa kufananisha Democrasia ya CHADEMA na ya Bunge ni, msisuse sasa na kutoka nje mkifanyiwa hivyo kwa sababu ni utaratibu wenu pia.
 
CDM is now a one man party serving the interests of the owner and not the interest of tanzanians.
 
Demokrasia ipi unayozungumzia haswa , je chama chako Kinafata demokrasia . Nianze na mifano michache swala la umeya Tanga ,Dar na morogoro ni demokrasia ipi mmetumia tatizo hapo Lumumba mmezidi kukurupuka . Kwa hiyo zile kura za ndio/ hapana kule Bungeni hazifati demokrasia? Toa borit kwenye jicho lako ndo utoe kitanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
KWANI KATIBA YAO (CHADEMA) IMEVUNJWA? NAOMBA UFAFANUZI ? KWANI BUNGENI WANAPOPIGA KURA ZA WAZI ZINAKUWA SAHH? TENA KWA KUSEMA NDIO AU HAPANA. JIBU UNAAMBIWA WALIOSEMA NDIO WAMESHINDA .........KIEGEZO SAUTI KUBWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…