DEMOKRASIA Kwa wajinga, wasiostaarabika, Wasiokuwa wazalendo yafaa nini?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
20,725
32,448
Salaam, Shalom!!

Nauliza tu,

Hawa waliotuletea DEMOKRASIA mataifa ambayo Bado tunajitafuta yalilenga nini?

Mbona wao walipokuwa wanajenga Uchumi wao, miaka mingi iliyopita mbona waliotumia mijeredi?

Yaani mtoto asiyetaka shule, mzazi ampe mtoto huyo DEMOKRASIA na uhuru Ili iweje?

DEMOKRASIA kumpa bodaboda uhuru ,asiye na lesseni anayeingilia njia ya mwendokasi makusudi yafaa ni ni?

DEMOKRASIA na uhuru usio na mipaka wa kumwachia mtoto achezee bunduki yenye risasi yafaa nini?

DEMOKRASIA Kwa wezi, waovu ,wabadhirifu yafaa nini?

Kwanini wanasiasa wote na watumishi wa umma wasipelekwe JKT Kwa lazima Kwa angalau miezi SITA wafundishwe Uzalendo Kwa viboko?

Yaani HAKI za binadamu Kwa Wasiokuwa wazalendo Kwa nchi Yao, Ina mchango Gani Kwa maendeleo yetu?

DEMOKRASIA ni ya nini Kwa wezi wa kura?

Yaani mtu auze msitu Kwa Mfano, alindwe na Sheria, mchakato uanze Polepole, kabla kesi haijaenda mahakamani, ameshahonga wote hapo juu, baada ya siku chache hakuna kesi, hakuna msitu!!

Swali: DEMOKRASIA Kwa wajinga Ina manufaa Gani?

OMBI: TULETEENI DIKTETA MWINGINE TAFADHALI!!!

Karibuni!!
 
Watanzania ni makondoo na wanafiki na wazembe tunahitaji Magufuli wa pili katili zaidi ainyooshe nchi...tukana uwezavyo lkn bila hivyo nchii ni kilema
Yaani waovu uwatangazie AMANI, Nchi itatawalika Kweli?
 
Hatukuletewa demokrasia, wakoloni walipoondoka tuliamua kurithi mifumo yao ya utawala badala ya kurudi kwenye mifumo ya machifu au wafalme.
 
Hatukuletwa demokrasia, wakoloni walipoondoka tuliamua kurithi mifumo yao ya utawala badala ya kurudi kwenye mifumo ya machifu au wafalme.
DEMOKRASIA Kwa mtu asiyekuwa na Elimu ya Uraia na UZALENDO wa kukataa kuhongwa unasaidia nini?

Turudi tukae na kupata wazo la pamoja kuipeleka Nchi yetu mbele.
 
Wakurugenzi wa halmashauri, Wakuu wa mikoa na wilaya ambao ni watu wenye nguvu kubwa sana nchi hii hawachaguliwi kwa kura wala kudhibitiwa na bunge au mabaraza ya madiwani.
 
Sasa sie DEMOKRASIA ya KAZI Gani,

Unachagua mbunge ,Rais ambaye huwezi kumfuta KAZI ya nini DEMOKRASIA hiyo?
Sahihi, Sisi tunapaswa kutafsiri Demokrasia kutokana na mazingira yetu halisi, na sio kuiga ile ya wenzetu. Bila hivyo hakuna tutakacho fanya cha maana.
 
Nchi gani za Africa ni mfano wa tawala za demokrasia halisi kwako?
Mimi sitaki kujifananisha Nchi yangu na majirani,

Nchi yangu ni ya kipekee sana. Afrika ije kujifunza hapa.
 
Nchi yetu inatakiwa tuwe na namna ya kuongoza nchi inayokubalika na wananchi wetu . Hii tabia ya kuiga iga na kujilinganisha sio nzuri na haina afya njema . , eti nchi fulani imekopa sana kuliko sisi , mara nchi yetu inakopesheka akati mikopo yenyewe haiwaletei unafuu wowote wananchi zaidi ya nchi kuja kupigwa mnada na pia viongozi wanaifisadi mikopo yenyewe haifikii malengo tarajiwa .

"Democracy is not a bottle of coca cola which you can import . Democracy should develop according to that particular country." - Julius Nyerere
 

Attachments

  • Screenshot_20240617-184009.jpg
    37.7 KB · Views: 2
Labda hujui maana ya demokrasia
Demokrasia haiondoi utawala Sheria na maadili ya utu

Rudi tena shule jifunze demokrasia inavyooperate


Mimi na walio wengi watafiti na wanazuoni tunaikubali demokrasia kuwa ni mfumo mzuri wa utawala duniani kwa jamii mchanganyiko kama za kwetu

Sijui wewe mwenzetu kwa utafiti wako ni mfumo Gani wa utawala unaona unafaa
 
Demokrasia ni kama ilivyo dini tu.
Wapo Watu wanaichafua dini vivyo hivyo kwa demokrasia

Demokrasia haijawahi kuwa tatizo labda tatizo ni watu wenyewe
 
Dictator labda la kizungu ,bongo wachumia tumbo tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…