Deborah Fernandez ni mchezaji wa kawaida Sanaa, Simba Bado timu haijakaa vizuri tunajipa moyo tu

Metronidazole 400mg

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
788
1,790
Kwanza kabla ya yote namshukuru Mungu Huwa nikileta mada hapa jamii sports, kwa mara ya kwanza watu Huwa wanaichukulia tofauti ila baada ya mda ukweli unadhibitika!!. fuatilia mada zangu za humu jamii sports utanielewa.

Sasa twendeni sambamba kwenye mada husika kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyoeleza

Deborah Fernandez ni mchezaji ambaye Simba imemsajili miongoni mwa maingizo mpya misimu huu ila ulishawahi jiuliza kwanini ghafla sikuizi hapati nafasi?? na mara nyingi anaanzia benchi?

Huyu mwamba naweza kusema kwa pale Simba kwenye nafasi yake ambaye pia wapo watu kama okejepha, Ngoma, mzamiru na kagoma....yeye ndio mchezaji mwenye mchango mdogo kuliko hao wenzake kwanini??

Huyu jamaa sifa yake kubwa ni kufanya interception ya mipira TU, sio mzuri kwenye kupanda as box to box....Wala sio mzuri kwenye kupiga pasi sahihi ( mara nyingi pasi zake zinapotea kirahisi, usibishe fuatilia ), hivyo Hana sifa ya kuwa central midfielder.....kidogo kwenye DM (Defensive midfielder) anajitahidi kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufanya interception ila ni kwa asilimia kama 45% TU.

Kocha fadlu kumuanzisha Fernandez benchi sio kwa bahati mbaya ila Kuna vitu jamaa hampi ndio maana mara nyingi ana opt kuanza na okejepha na Ngoma.....Ngoma mzuri kwenye kupiga pass za hatari, okejepha mzuri kwenye interception na kufanya maamuzi ya haraka....hivi vitu kwa hawa wachezaji wawili Fernandez

Hana kabisa na ndio inanifanya kuanzisha hii thread, sio kwa chuki Wala kushurutishwa Bali ni kuona na kuutazama mpira kwa jicho la tatu

Mwisho, kama umeelewa hayo maelezo hapo juu, utakubaliana nami kuwa, Simba Bado shida kubwa IPO kwenye kiungo wa chini.....ahoua mnambebesha mzigo Bure TU!!!!

Wale viungo wawili wa chini Bado hamna mutual combination kabisa....kocha anachofanya nikujaribu TU nani akicheza na nani angalau ila tiba Bado haijapatikana

Mpaka Leo ni zaidi ya misimu mitatu tumekosa kabisa kiungo mkabaji asilia, tuliaminishwa okejepha, ila ni kiungo mkabaji asilia??? ( Ni uongo si ndio??? na mpira haudanganyi ).....angalau yufuph kagoma ila naye pancha nyingi sio wa kumtegemea Toka tupo Singida..

Mambo ni mengi mda mchache, ila kiufupi na kumalizia Simba Bado haijakaa vizuri kama wengi tunavyoaminishana, Tuombeane uzima TU na haya maoni viongozi wa Simba popote walipo wayachukue na kuyafanyia kazi.......NIMEMALIZA

remember the post 29/11/24
 
Bora ya huko msimbazi sisi wa jangwani ndio kabisa.
Kosa kubwa kumfukuza kocha....hakika mmekosea sana.....hamna natural wingers wakutegemea mnatoboaje.....Huwa nikiwaza hili la wingers halafu puuup!! Kocha katimuliwa Ile akili Aya kumchukulia Hersi kama genius inapotea kabisa.....kwann asingesubiri dirisha dogo??
 
Kwanza kabla ya yote namshukuru Mungu Huwa nikileta mada hapa jamii sports, kwa mara ya kwanza watu Huwa wanaichukulia tofauti ila baada ya mda ukweli unadhibitika!!.......fuatilia mada zangu za humu jamii sports utanielewa.

Sasa twendeni sambamba kwenye mada husika kama kichwa Cha habari hapo juu kinavyoeleza

Deborah Fernandez ni mchezaji ambaye Simba imemsajili miongoni mwa maingizo mpya misimu huu.....ila ulishawahi jiuliza kwanini ghafla sikuizi hapati nafasi?? na mara nyingi anaanzia benchi???

Huyu mwamba naweza kusema kwa pale Simba kwenye nafasi yake ambaye pia wapo watu kama okejepha, Ngoma, mzamiru na kagoma....yeye ndio mchezaji mwenye mchango mdogo kuliko hao wenzake kwanini??

Huyu jamaa sifa yake kubwa ni kufanya interception ya mipira TU, sio mzuri kwenye kupanda as box to box....Wala sio mzuri kwenye kupiga pasi sahihi ( mara nyingi pasi zake zinapotea kirahisi, usibishe fuatilia ), hivyo Hana sifa ya kuwa central midfielder.....kidogo kwenye DM (Defensive midfielder) anajitahidi kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kufanya interception ila ni kwa asilimia kama 45% TU.

Kocha fadlu kumuanzisha Fernandez benchi sio kwa bahati mbaya ila Kuna vitu jamaa hampi ndio maana mara nyingi ana opt kuanza na okejepha na Ngoma.....Ngoma mzuri kwenye kupiga pass za hatari, okejepha mzuri kwenye interception na kufanya maamuzi ya haraka....hivi vitu kwa hawa wachezaji wawili Fernandez Hana kabisa na ndio inanifanya kuanzisha hii thread, sio kwa chuki Wala kushurutishwa Bali ni kuona na kuutazama mpira kwa jicho la tatu

Mwisho, kama umeelewa hayo maelezo hapo juu, utakubaliana nami kuwa, Simba Bado shida kubwa IPO kwenye kiungo wa chini.....ahoua mnambebesha mzigo Bure TU!!!!

Wale viungo wawili wa chini Bado hamna mutual combination kabisa....kocha anachofanya nikujaribu TU nani akicheza na nani angalau ila tiba Bado haijapatikana

Mpaka Leo ni zaidi ya misimu mitatu tumekosa kabisa kiungo mkabaji asilia, tuliaminishwa okejepha, ila ni kiungo mkabaji asilia??? ( Ni uongo si ndio??? na mpira haudanganyi ).....angalau yufuph kagoma ila naye pancha nyingi sio wa kumtegemea Toka tupo Singida..

Mambo ni mengi mda mchache, ila kiufupi na kumalizia Simba Bado haijakaa vizuri kama wengi tunavyoaminishana, Tuombeane uzima TU na haya maoni viongozi wa Simba popote walipo wayachukue na kuyafanyia kazi.......NIMEMALIZA

remember the post 29/11/24
Mbona Utopolo mna matatizo hivi ? Sisi wanaSimba wote tunaelewa timu yetu bado haijakaa sawa
 
Mashabiki sijui tunatatizo gani,ujuaji mwingi ,hata ungeambiwa umlete mchezaji unayemtaka na unapewa uwezo wa kifedha wa kumleta baada ya mda unaweza kumfukuza mwenyewe. Hakuna mchezaji aliyekamilika kama Fernandes ana mapungufu kiasi hicho ni mchezaji gani sasa pale Simba anafaa? Hebu tupunguze ujuaji wa kila kitu.
 
Kumshambulia mtu personal Badala ya hoja ni kutokuwa mkomavu kifikra mchallage mtu Kwa hoja
 
Kosa kubwa kumfukuza kocha....hakika mmekosea sana.....hamna natural wingers wakutegemea mnatoboaje.....Huwa nikiwaza hili la wingers halafu puuup!! Kocha katimuliwa Ile akili Aya kumchukulia Hersi kama genius inapotea kabisa.....kwann asingesubiri dirisha dogo??
Hata mimi ilo linanishangaza sana, walikurupuka kumtimua gamondi.
 
Hujui mpira man, Fernandes ni mchezaji mzuri, mechi alizocheza hovyo hazizidi 3,huenda kuna tatizo la kinidhamu au mastarehe ya bongo yameanza kumlevya. Si kila mchezaji anaweza kuzishinda starehe za Dar, yuko wapi Mo Ibrahim na kipaji kikubwa alichokuwa nacho? Kocha amedhihirisha ni kocha mzuri hata kuwaweka bench akina Ateba na Debora kwa sababu anawajua zaidi na ni njia ya kuwataka wajitathmini
 
Timu karibu yote ni mpya haiwezi kuwa vizuri Kwa haraka kama watu wanavyojitapa, sema at least unaona Kuna Fulani na Fulani watatufaa, Fulani naona hawatufai...ni mfano wa kapu la maembe, unachagua mazuri na mabaya unaweka kando.
 
Ni ukwel mtupu...jamaa karbia 80% pass zake c accurate...na Zaid ana dribbling za kizaman ambacho zinachukuliwa tu mguuni kirahisi....kocha ana haki kumkalisha mbao ndefu
 
Simba bado inajijenga ila ingalao graph yake inapanda sasa huko kwa wajivuni wanaotaka waletewe timu toka mbinguni kila siku graph inashuka lakini hawataki kukubali ukweli huo.
 
Back
Top Bottom