Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,509
- 4,776
Hivi unaukumbuka mkasa ulioitikisa Kilabu cha Inter pale walipo msajili Ronaldo de Lima maarufu huko Itaguai Nchini Brazil kwa jina Elgodo yaani Bwanyenye?!
Inter walimsajili Phenomeno kwa kitita kirefu sana cha pesa.
Usajili wa huyu mwamba hakika ulitikisa Dunia.
Usajili huu uliibua pande mbili Kilabuni hapo kiasi kwamba kuna Watu waliupokea kwa Mikono Miwili na kuna kundi la Watu waliukataa usajili huo.
Walioukataa usajili huo walikuja na utetezi kwamba tayari Kilabuni hapo kuna Mwamba ambae aliwatosha kwenye huduma ya upachikaji wa mabao.
Kundi hili lilisimama na Mvamizi Ivan Zamora Zamorano maarufu kama Bam Bam na kusema huyo Mtu alikuja Kilabuni hapo kwa mapenzi ya dhati akikubali kuiacha Real Madrid na kujiunga nao.
Lakini kundi jingine walisema De Lima ndie anafaa kuwa Nyota wa Kilabu hicho na ndie star wa Timu.
Kundi hili liliongozwa na mmiliki mtata wa Kilabu hicho Bilionea wa visima vya Mafuta Masimo Moratti.
Mpasuko mkubwa ulikuja kuibuka kwenye sakata la kupewa namba za Mgongoni katika Jezi.
Bam Bam aling’ang’ania kubaki na namba yake 9 Mgongoni huku Elgodo akisisitiza kupatiwa namba 9 Mgongoni ili aweze kutoa huduma ipasavyo Kilabuni hapo.
Sakata hili lilipelekea kucheleweshwa kupigwa Picha ya Pamoja ya Kilabu mwanzoni mwa msimu, huku Mvutano ukiwa mkubwa na kupelekea kuigawa Timu.
Mwisho wa Siku washauri wa Zamorano kutoka Santiago Chile walimtuliza Kijana wao na kumwambia akubali kuiachia namba hio lakini kwa Masharti ya kupewa namba 18 yenye alama ya Jumlisha katikati ikisimama kama 1+8 ambayo jawabu lake ni sawasawa na 9.
Sakata kama hilo likataka kujirudia katika Klabu ya AC Milan pale Mtume na Nabii wa Mwisho wa Mchezo wa Soka Ronaldinho Dinho Gaucho alipo tua klabuni hapo na kutoa ombi la kupewa jezi namba 10 aliokuwa akiivaa klabuni Barcelona na hata timu ya Taifa ya Brazil.
Unajuwa kwa wakati huo Klabuni Milan jezi namba 10 ilikuwa ikivaliwa na nani?!
Na jibu alilo pewa Gaucho aliambiwa nini?!
Unajuwa kwanini Dinho aliamua kuvaa jezi namba 80?!
Endelea kunywa Mtori, Nyama utazikuta chini.
@acmilan_swahili⚫️🔴