beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,880
6,365
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amedai kuwa uchunguzi uliyofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kwamba Hamza Mohammed alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga.

Hamza aliuawa na polisi Agosti 25, mwaka huu baada ya kuwaua kwa risasi askari wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi jirani na ulipo ubalozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Alhamisi Septemba 2, 2021 jijini Mwanza na waandishi wa habari Wambura amesema uchunguzi huo ulijikita katika mambo makuu matatu ambayo ni kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma Hamza kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi.

"Amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kwa kuangalia mitandao ambayo inaonyesha matendo ya Al-Shabab na makundi kama ISIS yanayoendelea na wagaidi wengi hujifunza kupitia mitandao hiyo," amesema Wambura.

Amesema kwamba kitendo alichokifanya Hamza kilikuwa ni cha ugaidi wa kujitoa mhanga.

"Tabia na matendo ya Hamza aliyapata kupitia mawasiliano aliyokuwa nayo na watu wanaoishi katika nchi zenye matendo ya kihalifu ikiwemo ugaidi hasa wa kupitia mtandao yanayojulikana kama "Radicalisation through social media)," amesema Wambura.

Kuhusu taarifa zinazodai kwamba Hamza aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake, Wambura amekanusha na kusema katika uchunguzi huo wamebaini kwamba Hamza hakuwa na madini wala fedha katika mazingira yale.

"Hamza hakuwa na madini wala pesa na hakuwa katika nafasi yoyote ya kumiliki madini wala pesa mbali ya kwamba watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu," ameongeza Wambura.

Wambura ameongeza kuwa taarifa ya uchunguzi huo pia imebaini kwamba Hamza alikuwa kwenye kundi la magaidi wanaoamua kuifia dini.

Chanzo: Mwananchi
 
Ridiculous😁
Ile intelijensia ya polisi ya fujo kwenye mikutano ya CHADEMA ilikuwa wapi mpaka Hamza akawa gaidi na huku ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya?
Ile intelijensia ya polisi ya fujo kwenye mikutano ya CHADEMA ilikuwa wapi mpaka Hamza akawa gaidi na huku ni mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya?
 
"Wambura amesema katika uchunguzi huo polisi imebaini kwamba Hamza alikuwa akiishi kisiri huku akiwa amegubikwa na viashiria vyote vya ugaidi"

Halafu intelijensia ya polisi haikuwa ikijua siku zote hizo? Ili hali mikutano ya ndani ya vyama vya upinzani hata kabla haijapangwa tayari wanakuwa washajua na kuzuia basi jeshi letu lina walakini
 
Huyu DCI anatugeuza wote kuwa ni vilaza,kama kweli uchunguzi umefanyika vielelezo vipo wapi?vya kumthibitisha kuwa Hamza(rip)alikua ni gaidi.

kwanza ile crime scene ilishakua contaminated na raia waliovaa uniforms,polisi wanajichunguza wapi umeona kwenye dunia hii? Hapa ilibidi ipid (sisi hatuna na wamefanya haya kwa makusudi )ndio wangefanya uchunguzi huu bcs police nao walikua sehemu ya suspects.

Maiti inapigwa risasi nyingi unnecessary inatia uchungu mno,time ni mwamuzi mwema na shame on you DCI kama unaingia kwenye nyumba za ibada.
 
Aisee siwez kubisha sana..lakini kwa Mtanzania tu aliyekulia katika mazingira ya kitajiri hawez kuwa anajua kushika bunduki vile na kujiamini kiasi kile kwa umri ule...palikua na namna..na inawezekana kabisa ametuma salam kwa wenzake..inaweza kuwa mwanzo wa ugaid tanzania au mwisho wa ugaid inategemea tu na vyombo vya usalama vitakavyolimaliza hili
 
Back
Top Bottom