upupu255
Senior Member
- Sep 4, 2024
- 166
- 180
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Nyakia Ally Chirukile amekemea vikali ubadhilifu unaofanywa na watumishi wanaotekeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege Sumbawanga.
Akizungumza na wafanyakazi hao Machi 21, 2025 wakati wa ziara ya kushtukiza Chirukile amesema kuna ubadhilifu unaofanywa na baadhi ya viongozi kwa kushirikiana na wafanyakazi kuhujumu malighafi inayotumika katika ujenzi wa uwanja huo.
Chirukile, amesema Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaoiba na kuhujumu vifaa vya ujenzi katika eneo la mradi.
"Nataka niwaambie kuwa Serikali ipo kazini haijalala, kuna wizi unaendelea, na ubadhilifu unafanyika hapa wapo viongozi wanashirikiana na baadhi ya wafanyakazi kuiba vifaa hasa saruji na mafuta na hii tabia inakwamisha mradi wetu kushindwa kukamilika kwa wakati, miradi hii ni ya Watanzania wote na fedha hizi ni za Watanzania walipa Kodi," amesisitiza Chirukile.
Pia amesema wizi huo unakwamisha mradi kukamilika kwa wakati uliopangwa, Serikali haitamfumbia macho mtu yoyote anayejihusisha na kuiba vifaa katika eneo la mradi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Joseph Gimonge amesema wameendelea kuchukua hatua kwa baadhi ya watumishi ambao wameshindwa kutekeleza majukumu yao ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Gimonge amesema ujenzi wa uwanja wa ndege unaendelea ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu.
Naye, Jackline Mbalaga ambaye ni Afisa Utumishi wa BCEG amesema wapo baadhi ya watumishi wenye tabia ovu za wizi wa vifaa katika eneo hilo na kwamba wameendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wale ambao wanajihusisha na tabia ovu ikiwa ni pamoja na kuwapeleka katika vyombo vya sheria.