Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,049
- 2,717
Wakuu,
Hivi badala ya kutumia social media, redio na TV au njia nyingine za kufikia wananchi unaamua kwenda kufanya Marathon kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi?
Vihoja hivi utavipata Tanzania tu. Sijawahi kusikia nchi nyingine kama Marathon zinasaidia kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye Uchaguzi.
Na hii sio Tabora tu nimeona pia kuna mikoa mingine kuna marathin zinaendelea kuhamasisha ushiriki wa wananchi. Hii ni strategy mpya? Nani analipia hizo marathon?
Huyu DC wa Tabora inabidi atueleze hizo pesa za kuandaa hiyo Marathon katoa kwenye bajeti gani? Au ni mshahara wake?
===================================================
Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Mhandisi Deusdedith Katwale, amewahimiza wakazi wa Tabora kushiriki kikamilifu katika kampeni za vyama vya siasa na uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024, ili kuchagua viongozi watakaokuza maendeleo.
Akizungumza wakati wa zoezi la uhamasishaji lililofanyika Manispaa ya Tabora, ambalo lilijumuisha michezo ya mbio na mazoezi ya viungo, Katwale alisisitiza ushirikiano wa wakazi, viongozi wa serikali, na taasisi mbalimbali katika maandalizi ya uchaguzi.
Source: Jambo TV