BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 500
- 1,209
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dkt. Vicent Mashinji ametoa siku 7 kwa viongozi wa siasa waliowaambia wafanyabiashara warejee katika maeneo yao ya awali ya biashara na kuondoka katika maeneo yaliyotengwa, kwenda kukanusha kauli zao vinginevyo atawachukulia hatua kali za kisheria.
“Niwaagize wote mliokuwa mmeenda kutoa kauli hizo (wafanyabiashara kurejea kwenye maeneo ya awali) nendeni mkazikanushe haraka kabla hatua kali hatujawachukulia.
“Haiwezekani wananchi tunawawekea eneo maalum ninyi mnaenda kupotosha,“ - Dkt. Vicent Mashinji.
Chanzo: Dar Mpya