Egnecious
JF-Expert Member
- Jul 8, 2015
- 879
- 969
DC HAPI KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KINONDONI LEO MUUNGANO DAY
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Salum Hapi leo tarehe 26/04/2016 ambayo ni siku ya maadhimisho ya miaka 52 ya Muungano anafanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo iliyoko manispaa ya Kinondoni ambayo itazinduliwa na Mwenge.
Mh. Hapi ameagiza wakuu wa idara za uchumi, miradi, injinia wa barabara, maji na Mkurugenzi wa manispaa kufika ofisini leo tayari kwa zoezi hilo. Ziara hiyo inalenga kukagua miradi hiyo na kuona kama inalingana na thamani ya fedha iliyotajwa (value for money).
Hadi saa 1 kamili asubuhi Mkuu huyo wa wilaya alikua amewasili ofisini tayari kwa ajili ya majukumu.
Miradi inayotarajiwa kukaguliwa ni pamoja na Soko la Mburahati, ujenzi wa barabara ya Arsenal - Magoti Saranga, ujenzi wa wodi ya wazazi Ubungo, ujenzi wa hostel na kalavati Mabwepande na ujenzi wa kisima cha maji Makongo.
Huu ni muendelezo wa kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ya Rais Dr. John Magufuli ambayo haiangalii sikukuu wala siku za mapumziko katika kuwatumikia wananchi.