Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,717
- 13,467
Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kueleza kuwa kuna changamoto kubwa ya foleni eneo la Busisi kwa Watu wanaohitaji kuvumia kivuko kuvuka tangu usiku wa kuamkia jana Agosti 29, 2024, akidai Kivuko hakifanyi kazi, upande wa Serikali umeeleza kinachoendelea.
Mwanachama huyo alidai hali hiyo imesababisha kero kubwa ya Watumiaji kuchelewa katika shughuli zao, anatoa wito wanaohusika warekebisho changamoto ya kivuko iliyojitokeza ili huduma irejee kama kawaida.
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Kivuko eneo la Busisi na Kigongo ferry hakifanyi kazi 24hrs
=====
JamiiForums ilipomtafuta Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga kuhusu madai hayo amesema “MV. Sengerema ina matatizo kidogo katika mfumo wa injini, vivuko vingine viwili (MV. Mwanza na MV Misungwi), kwa kuwa imezoeleka vinapishana na leo Ijumaa kuna idadi kubwa ya watu ndio maana changamoto hiyo imetokea.
Ameongeza “Upande mwingine kuna njia mbili, kuna Kamanga Ferry, wao wanaendelea na huduma kama kawaida. Hivyo, wakirekebisha MV Sengerema vyote vitakuwa vinafanya kazi, kwani hata MV Mwanza nayo juzi ilileta shida na baadaye ikakaa sawa.”