the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 566
- 816
Jumla ya Vikundi 52 vya wajasiriamali wadogowadogo wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro vimekabidhiwa Mkopo wa Jumla ya Shilingi Milioni 641 unaotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya hiyo.
Zoezi lakukabidhi mikopo hiyo limefanyika leo Jumatano April 16, 2025 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Rombo ambapo Mkuu wa wilaya hiyo Mwl. Raymond Mangwala amevikabidhi vikundi hivyo kwa niaba ya Halmashauri hiyo.
Akikabidhi Mikopo hiyo kwa vikundi hivyo ambavyo ni vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu Mkuu huyo wawilaya amewataka wanavikundi hao kuzingatia taratibu za mikataba katika urejeshaji wa mikopo husika huku akiwataka wanavikundi hao na vikundi vingine kuhakikisha kuwa vinashiriki mafunzo ya ukopoaji, matumizi na urejeshaki wa mikopo hiyo.
Mbali na hayo pia amewataka kuwa wakweli pindi wanapoandaa na kuandika andiko la miradi yao kwani wanavikundi wengi wamekuwa wakikosa sifa zakupata mikopo kutokana na kuwa wadanganyifu kwenye maandiko ya miradi.
Pia amewataka kuhakikisha kuwa wanafuata malengo ya mikopo waliyoichukua na siyo kwenda kinyume kwani watashindwa kurejesha.