DC Lindi Amulika Miradi ya Elimu, Asisitiza Muda, Ubora na Thamani ya Fedha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,591
1,191

DC LINDI AMULIKA MIRADI YA ELIMU, ASISITIZA MUDA, UBORA NA THAMANI YA FEDHA

Mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amesisitiza Miradi ya elimu kukamilika kwa wakati, Ubora na thamani ya fedha ambapo ameyasema hayo akikagua miradi ya Elimu Sekondari katika Manispaa ya Lindi akianza na Miradi kikubwa mitatu ya Kielimu ambayo ni zaidi ya Bilioni 1.5 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia Mradi wa Sequip III.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa shule ya Sekondari Dr Jakaya Kikwete inayojengwa Kata ya Nangaru- Manispaa ya Lindi, ambayo itagharimu jumla ya shilingi 560,552,827/= , Mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Hamida Alqassim kata ya Rasbura- Manispaa ya Lindi wa jumla ya shilingi 560,552,827/= na Shule ya sekondari Kitomanga - Kata ya kitomanga yenye jumla ya fedha 515,000,000/=

Aidha katika ziara hiyo DC Mwanziva amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kushusha fedha hizi katika Manispaa ya Lindi na kuahidi usimamizi bora, ufuatiliaji, thamani ya fedha, ubora wa miradi ili iweze kutoa huduma thabiti.

Miradi hii ipo katika hatua tofauti za utekelezaji na nguvu kubwa imewekwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na kutoa huduma.

Katika ziara hiyo ya kikazi, Mkuu wa Wilaya aliambatana na Mkurugenzi wa manispaa ya Lindi Bw. Juma Mnwele wakiongozwa na mkuu wa idara ya elimu sekondari Manispaa ya Lindi Bi. Rehema Nahale, pamoja na maafisa wengine toka idara ya Elimu Sekondari na Idara ya Ujenzi Manispaa ya Lindi kwa lengo la kuwa na usimamizi wa pamoja na matokeo bora ya miradi hii.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.57.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.57.jpeg
    148.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.57 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.57 (1).jpeg
    131.4 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58.jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58.jpeg
    161.1 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58 (1).jpeg
    101.8 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58 (2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-12-13 at 14.47.58 (2).jpeg
    129.1 KB · Views: 1
Back
Top Bottom