falcon Q
JF-Expert Member
- Feb 28, 2023
- 925
- 2,465
Wananchi wa Kijiji cha kisimiri Juu wilaya ya Arumeru wamepewa siku saba kung'oa miche ya bangi katika mashamba yao baada ya kubainika kuendelea na kilimo hicho licha ya kupigwa marufuku.
Kubainika kwa mashamba hayo katika Kijiji hicho kumetokana na operesheni iliyofanywa na kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya Wananchi iliyofanyika June 11, 2023 na kufanikiwa kung’oa hekari 60 za zao hilo.
Maagizo hayo yamekuja takriban siku tatu tangu operesheni nyingine iliyofanywa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) iliyoongozwa na Kamishna Jenerali Aretas Lyimo katika vijiji vya Arumeru ambapo gunia 931 za Bangi zilikamatwa Arumeru.
Katika operesheni hiyo iliyofanyika kijiji cha Lesinoni na maeneo ya jirani pia hekari 953 za bangi ziliteketezwa na ilibainika uwepo wa bangi mbichi gunia 4,975 na watu 16 walikamatwa.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda akizungumza wakati wa operesheni Kijiji Cha Kisimiri ameonya baadhi ya wananchi kuendelea kwa Kilimo hicho na kutoa siku Saba kung'oa bangi mashambani.
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifaView attachment 2654291