Day 2: Mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Dodoma, Septemba 5, 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,828
13,585
04.jpg

Screenshot 2024-09-05 162313.png
Mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (Annual Non-Government Organizations Forums), Jijini Dodoma, unaelekea leo Septemba 5, 2024 ikiwa ni siku ya pili yhangu ulipoanza.

Mkutano huo ambao unafanyika kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete umepangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo leo ikiwa ni siku ya pili ambapo unatarajiwa kufikia tamati Septemba 6, 2024.

Mshauri wa Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Jukwaa la Kizazi chenye usawa, Angellah Jasmine Kairuki ni mmoja wa washiriki kwenye Mkutano huu.
Hajjat Mwantumu Mahiza
Akizungumza katika Mkutano huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Hajjat Mwantumu Mahiza, amesema:

Nafasi ya NGO kwenye Nchi yetu ni kubwa, wanafanya mambo makubwa, ni wajibu wetu kuendelea kushirikiana nao katika kuendeleza maendeleo ya Nchi yetu.
01.jpg
Mgeni Rasmi – Amon Anastaz Mpanju
Mgeni Rasmi wa Siku ya le oni Naibu Katibu Mkuu – Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum, Amon Anastaz Mpanju, anazungumza:

Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yamekuwa na umuhimu mkubwa kwenye Jamii na yanafanya kazi kubwa ndio maana yamekuwa yakipewa ushirikiano na Serikali.

Mpaka leo (Septemba 2024) Mashiriki Yasiyo ya Kiserikali ambayo yamesajiliwa na yapo ‘active’ ni 9,857 ambayo yanajihusisha na sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, nishaji, Maji, Mazingira, hifadhi ya mazingira na mengine mengi.

Natoa wito NGO’s mnatakiwa muendelee kuzingatia Uwajibikaji, Uzalendo na utekelezaji wa majukumu kwa misingi inayotakiwa.

Mtanatakiwa kuzingatia weledi, Uwajibikaji, Sheria na Kanuni zinazowaongoza.

Pamoja na kufanya kazi kubwa na kusaidia Jamii, wapo baadhi yetu ambao kwa kuzingatia maslahi ya kifedha au maslahi yao binafsi wamekuwa wakichagua juhudi zenu na kutaka kuwagombanisha na Serikali.

Sisi Serikali ukikiuka au kwenda kinyume na utendaji wako tutachukua hatua hata kama ushiriki wako unanufaisha Watu wengi kwenye Jamii, hatutaenda moja kwa moja kufuta taasisi, tutakuita tutazungumza, tutajadiliana nini kimetokea, usitulazimishe kufika hatua ya kufuta taasisi yako.

Tanzania ndipo nyumbani kwetu, amani utulivu na maendeleo yataletwa kati ya mimi na nyie, kumbukeni kuwa chochote mnachokifanya msiwe mnaendeshwa na upepo wa Kisiasa.

Tuzingatie maadili na misingi ya kazi yetu, nyie ni jicho la Serikali kwakuwa Serikali inawatengenezea mazingira wezeshi.
Screenshot 2024-09-05 162607.png
Mshauri wa Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa, Angellah Jasmine Kairuki
Screenshot 2024-09-05 161806.png
Wakili Fulgence Massawe
Mkurugenzi wa Uchechemuzi na Maboresho wa Kituo cha Sheria Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Fulgence Massawe

Tuboreshee mifumo wa Kisera ili iweze kuendana na wakati husika na mazingira badala ya kuwa na Mfumo wa Katibu, Mwenyekiti na Mkurugenzi.

Mwaka 2018 tulitengenezewa Kanuni zinazosimamia Uwajibikaji, pia Sheria zote zilizopo zimelenga kuleta na kutekeleza Uwajibikaji.

Kuendesha NGO kunatakiwa kuwe na fursa za kutambulika, bila kutambulika huwezi kupata maendeleo.

Kutambulika na Sheria ni fursa mojawapo kwa NGO, inaleta ushirikiano mzuri wa Serikali na Wadau wa maendeleo.

Kuna baadhi ya Mashirikia yanakuwa na changamoto kwenye iuwajibikaji

Stephen Motambi
Stephen Motambi kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI anasema: NGO ni lazima zisajiliwe kwa mujibu wa Sheria ili kuwa na utendaji mzuri.

Serikali tunahamasisha ushiriki katika shughuli za maendeleo, tunawashirkisha Wananchi kwa kuwa tunatambua uwezo wao na mchango wao.

Tunatoa wito kwa Wadau kushirikiana na Wananchi wakati wanapokuwa na miradi mbalimbali ili hata mwisho wa mradi Wananchi wanakuwa na uwezo wa kuendelea katika kufanya shughuli zinazoendana na Mradi au zinazohusisha Mradi.

Ushirikishwaji wa Wananchi katika Miradi unasaidia kupunguza gharama mbalimbali za kutekeleza shughuli za Kiserikali.

TAMISEMI tumetengeneza muongozo ya kushughuli za Kiserikali, miongozo inapatikana katika tovuti ya TAMISEMI.

Pia kuna Mfumo tunaotumia unaoweza kutumiwa na NGO kujua mwenendo wa shughuli za Wananchi.

Kuna baadhi ya Watu wanafikiri Serikali peke yake ndio inaweza kutoa maendeleo, ukweli ni kuwa kwa ushirikiano wa pamoja ni rahisi kupata maendeleo kwa kasi.

Kuhusu mfumo wa ufuatiliaji ni mfumo jumuishi unaohusisha idara na sekta mbalimbali, TAMISEMI tumeweka viashiria ambavyo vinashirikisha Wananchi, sekta nyingine pia zimeweka viashiria vyao lakini taasisi zote zinaweza kuingia kuona viashiria.

Blandina Nkini
Afisa Maendeleo ya Jamii, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Blandina Nkini anasema: Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Yapo ya aina mbili, kuna yale makubwa na madogo, changamoto nyingi ni kwenye mashirika madogo.

Changamoto mojawapo ni kuwa unakuta kuna Watu wanasajili lakini hawajui Sera na Sheria zinazoongoza kile wanachokifanya, wanakuwa na uelewa mdogo.

Mtu anaweza kuanzisha NGO, baadaye anakuja kugundua kuwa anatakiwa kujisajili na kulipa kodi, pia wengi wao wanaoanzisha au kusajili Mashirika hayo, hawasomi Sheria za Nchi na miongozo ya Nchi kuhusu Mashirika, pia wengi wao hawasomi Katiba zao.

Hajui anatakiwa kufanya kazi vipi na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) au Wizara husika, mwingine anashindwa kutambua kazi zake zinaendana na Majukumu ya Serikali.

Unaweza kumuuliza swali ambalo lipo ndani ya Katiba yake anashindwa kujibu, unakuja hajui tofauti ya Founder, member au Boad Member kiasi kwamba wanashindwa kuwa na utekelezaji wa kueleweka.

Ni mashirikia machache ambao unakuta wana Mhasibu mwenye sifa ya CPA, ukikuta hivyo mara nyingi ni maelekezo ya mfadhili, lakini wengine wanaajiri Watu ambao hawana sifa.

Kuna wachache wanashindwa kufanya majukumu yao ya msingi kisha wanageuka kuwa wanaharakati.

Ikitokea hivyo, huyo mwenye Shirika anaanza kukwepa Watu wa Serikali kwa kuwa anajua akikutana nao kibao kitamgeukia na anaweza kukutana na adhabu.

Hiyo ni kwa kuwa kuna Watu wakisajili Shirika wanachukua zile katiba na kuzifunika, hawazitumii tena.

Mfano, Arusha kuna Mashirika zaidi ya 1,000 lakini ukiwaita kwenye vikao, mafunzo na semina hawatokei wakati wanajua ni mikutano muhimu kwa kazi zao za kila siku.

Israel Ilunde
Mkurugenzi Mtendaji wa The Youth Partnership Countrywide (YPC), Israel Ilunde anasema:

Tunatakiwa tutambue kuna Kodi na adhabu za TRA, kama TRA ikiamua kusimamia Sheria, NGOs nyingi zitapata wakati mgumu, hivyo kama haujajipanga bora usishiriki kwenye masuala ya NGO.

Changamoto nyingine ni kuwa Muongozo uliotumika katika Mashirika unaeleza kuwa Wizara inatakiwa kusimamia shughuli za NGO, hivyo inamaanisha shirika linahitaji kusimamiwa muda wote, ni vizuri mashirika yapewe nafasi ya kujisimamia ila yafuate muongozo.

Suala linguine ni kuhusu suala la kufuatilia kibali, kuna wakati kinachelewa kutokana na uwepo wa wingi wa Mashirika.

Nashauri kama inawezsekana Mashirika yangeachiwa wajibu wa kutoa taarifa kwa Serikali na siyo Mamlaka hiyo kuwendelea kushikilia jukumu la vibali ambalo limekuwa likisababishwa ucheleweshwaji wa Miradi mingi na majukumu mengine.

Jambo linguine muhimu ni kuwa TRA inatakiwa kutofautishe NGO na makampuni ya Kibiashara, kuwe na utaratibu wa kuongoza Mashirika katika masuala ya fedha tofauti na wenzetu weanaofanya biashara.
Hajjat Mwantumu Mahiza
Hajjat Mwantumu Mahiza ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anasema:

TRA haiwezi kubadili Sheria za kuongoza Mashirika, haina mamlaka ya kubadili chochote kwa kuwa Sheria ambazo mnazizungumzia zimetoka Bungeni.

Mwaka 2023, Makamu wa Rais alisema kuna dirisha la ushauri na maoni, tulienda tukatoa maoni na hoja zikawasilishwa katika njia zinazotakiwa, hivyo kutoka hapo TRA haiwezi kujiamulia yenyewe mabadiliko, kama tunataka mabadiliko tunatakiwa kuyasema kwenye mikuutano kama hii.

Wadau wa NGO kunapokuwa na nafasi ya kutoa maoni toeni maoni ili , mchakato ufanyike uende bungeni Sheria zipite, msione aibu au kujificha.

Kuhusu suala la NGO kupata fedha, kama pesa ulipata nyingi na huna maelezo, wakiziona zimeingia utakuja kuwapa maelezo, kuna mashirika yanapata fedha lakini kazi hatuzioni.

Mwanza kuna shirika linalohudumia Watoto liliingiza Shilingi Bilioni 7 kwa Mwaka lakini huduma zenyewe za Watoto hatuzioni, tulipoenda tukakuta kuna Watoto wana hali mbali wengine wanalala hadi juu ya miti

Mmiliki wa Shirika kazi yake ni kuwapiga picha na kupeleka kwa wafadhili ili apate hela, wakati mwingine anapiga picha Watoto wanaolala Vituo vya Mbasi na Vituo vya Daladala ili azitume picha apate hela.

Mtu anafanya hivyo kisha unaona Serikali inakuingilia.

Mfano mwingine kuna Shirikia linashughulikia walemavu limepokea zaidi ya Shilingi Bilioni 7 kwa Mwaka lakini mpaka leo hatujaona ilichofanya.

Ndugu zangu kuna mashirika yanahatarisha Nchi.

Zile nyumba mnazolea Watoto yatima mbona hatuoni waki-graduate, waliokuja awali wameenda wapi?

Biashara ya Watu imeshamiri (Human Traffick) tunaambiwa Watoto wamepelekwa kusoma ughaibuni mbona hatuwaoni na hatuambiwi maendeleo yao? Wanakwenda wapi?

Kibaya zaidi baadhi yenu hata ofisi hamna, nimeenda Mkoa flani kila tukimtafuta mwenye Shirika anaingia mitini kwa kuwa hana ofisi.

Pia soma ~ Biteko kufunga Mkutano wa Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, Dodoma, Septemba 6, 2024
 

Attachments

  • 22.jpg
    981.3 KB · Views: 4
Asante kwa Updates Mkuu. Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) yamekuwa na umuhimu mkubwa kwenye Jamii na yanafanya kazi kubwa ndio maana yamekuwa yakipewa ushirikiano na Serikali.
 
Back
Top Bottom