Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,814
- 13,580
Baada ya kudaiwa kuna changamoto ya huduma ya maji Mitaa ya Tabata hasa kuanzia Posta kuelekea Segerea, ikiwa ni wiki ya pili kuna uhaba wa maji huku Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ikiwa haitoi taarifa ya kinachoendelea, ufafanuzi umetolewa.
Awali ilidaiwa kuwa baadhi ya Wananchi wamefika ofisi za DAWASA Segerea lakini wanapewa majibu yasiyoeleweka
Meneja Mawasiliano DAWASA, Everlasting Lyaro amesema “Kulikuwa na matengenezo ambayo yameshakamilika ya Mtambo wa Ruvu Juu, lengo likiwa ni kuboresha huduma maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya kupata maji kidogo kutokana na mazingira yao ya Kijografia lakini tayari yameshaanza kutoka.”
Malalamiko ya awali soma hapa: DAWASA, Segerea kuna mgao wa maji kimyakimya? Wiki ya pili mitaani hakuna maji!