DAWASA: Tenki la ujazo wa lita milioni 9 la Bangulo lakamilika. Wakazi 450,000 kuhudumiwa.

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
618
866
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso, amewapongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kumaliza Mradi wa Maji wa Bangulo kwa Wakati huku akiwahimiza Wananchi Pugu Station wanaozunguka Tenki la Maji kulinda Mradi huo.
IMG-20250318-WA0046.jpg

Amesema hayo leo 18 Machi 2025 alipotembelea mradi wa maji eneo la Kusini mwa Mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama mradi wa Bangulo.

"Niwaombe, Mabomba haya na mradi huu ambao Serikali imewekeza fedha nyingi tuulinde kama mboni ya jicho. Ukiona mtu anakuja kuhujumu huyo hatutakii mema. Sitarajii na sitegemei kuona watu wanaunganishiwa maji kijanja janja mpaka atoe hela kiasi fulani hapana. Mtu ameomba kuanganishiwa maji ndani ya siku 7 aunganishiwe maji." Amesema Waziri Aweso.

" Ndugu zetu wasoma mita, ni marufuku kumbambikizia Mwananchi bili ya maji. Tunakwenda kubadili uelekeo juu ya Usomaji wa Mita. Tunaenda kuwa na mita za Luku ya maji. Ni marufuku kumkatia mtu yoyote maji siku ya sikukuu na Weekend". Ameongeza Aweso.
IMG-20250318-WA0027.jpg

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire, amemwambia Waziri Aweso kwamba kukamilika kwa Mradi huu kunaenda kumaliza na kupunguza tatizo la Maji katika eneo la Kisarawe(kata ya Kiluvya) na Majimbo matano ya Mkoa wa Dar Es Salaam ikiwemo Jimbo la Ukonga(Kitunda, Kipunguni na Kata ya Mzinga), Jimbo Segerea(Kinyerezi, Bonyokwa pamoja na Segerea), Jimbo la Ubungo(Kata ya Msigani pamoja na Saranga) Jimbo la Temeke(Kaya ya Buza, Yombo pamoja na kata ya Makangarawe).

"Kwa sasa hivi tupo kwenye Majaribio kuhakikisha kwamba wananchi sasa Wanapata maji ya uhakika. Tunaendelea na Majaribio haya ndani ya mwezi huu wa tatu hadi kufikia mwezi wa Nne. Wakati tunafanya majaribio Wananchi wanaendelea kupata maji." amesema Mhandisi Bwire

Mradi wa maji Bangulo umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 huku ukihusisha kazi za Ujenzi wa Tenki lenye ujazo wa lita milioni 9, Kituo cha Kusukuma Maji na Ulazaji wa bomba kwa umbali wa kilomita 119 na utahudumia wakazi wapatao 450,000 katika Kata za Mzinga, Kipunguni, Kitunda, Pugu station, Kiluvya, Msigani na Kinyerezi.

======

WAZIRI AWESO -SITARAJII WATU KUUGANISHIWA MAJI YA BANGULO KIJANJAJANJA

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwaunganishia maji wananchi watakaonufaika na Mradi wa Maji wa Bangulo kwa ufanisi na uaminifu na kuhakikisha hakuna mianya yoyote ya rushwa itakayojitokeza kwani kuunganishiwa maji ni haki ya msingi ya mwananchi.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Jumanne Machi 18, 2025 alipotembelea mradi huo uliopo mtaa wa Bangulo hali ya hewa katika kata ya Pugu Station wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, ukitazamiwa kunufaisha wananchi 450000 wa kata mbalimbali za wilaya hiyo na wilaya jirani.

"Sitarajii na sitegemei kuona watu wanaunganishiwa maji kijanjajanja mpaka atoe hela kiasi fulani ndiyo aunganishwe, hapana. Mtu ameomba kuunganishiwa maji, DAWASA ninaomba niwaeleze, ndani ya siku saba lazima mtu aunganishiwe maji," amesema Waziri Aweso.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amewaomba wananchi wa Bangulo kutunza vyema miundombinu ya maji katika eneo lao na kutoa taarifa watakapoona kuna dalili ya kuvuja kwa maji kutokana na baadhi ya mabomba katika eneo hilo kuwa ya muda mrefu. Amesema kwa kufanya hivyo, upotevu wa maji utadhibitiwa na huduma kwa wananchi itaendelea kutolewa kwa ufanisi.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama amesema mradi huo umegharimu jumla ya fedha za Kitanzania Shilingu bilioni 36.8 hii inajumuisha gharama ya ujenzi pamoja na usimamizi wa mradi ambapo kwa ujenzi pekee gharama ni Shilingi bilioni 35.0 na usimamizi wa mradi gharama ni Shilingi bilioni 1.8.

Amesema Dar es Salaam upande wa Kusini kulikuwa na changamoto ya maji kutokana na miundo ya kijiografia ya milima lakini kwa mradi huu, wananchi hawatapata shida tena kwani tayari kuna mitandao ya zamani ya maji katika eneo hilo ambayo inaendelea kuboreshwa na kutawekwa mtandao mpya.

Mradi huu unahusisha Manispaa za Ubungo, Temeke, na Jiji la Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma ya maji katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji ukilenga kunufaisha wananchi 450000 wa kata wilayani Ilala za Mzinga, Kipunguni, Kitunda, Pugu station na Kiluvya huku kata za Msigani wilayani Ubungo na Kinyerezi wilayani Ilala zikienda kuongezewa msukumo wa maji.
IMG-20250318-WA0040.jpg
IMG-20250318-WA0020.jpg
IMG-20250318-WA0051.jpg
IMG-20250318-WA0036.jpg
IMG-20250318-WA0044.jpg
IMG-20250318-WA0054.jpg
 
Zilonghwa mbali zitendwa mbali ,hao jamaa usiwaamini hata chembe ,tuliambiwa mradi wa bwawa la nyerere ukikamilika umeme utakuwa wa kutosha ila sasa umeme kila siku unakatika na mgao kila siku ,tanesco wanaomba kila siku kufanya maintanance lakini kila siku hitilafu kwenda mbele.

Walituambia mradi wa mwendo kasi mbagala utaanz mwezi wa 12 ila mpaka sasa haujaanza ,ilo bwawa hata kama lina uwezo wa kujaza lita bilioni 1 nina uhakika mgao wa maji utakuwa pale pale tena unaweza ukaongezeka.
 
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso, amewapongeza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) kwa kumaliza Mradi wa Maji wa Bangulo kwa Wakati huku akiwahimiza Wananchi Pugu Station wanaozunguka Tenki la Maji kulinda Mradi huo.
View attachment 3275062
Amesema hayo leo 18 Machi 2025 alipotembelea mradi wa maji eneo la Kusini mwa Mkoa wa Dar es Salaam maarufu kama mradi wa Bangulo.

"Niwaombe, Mabomba haya na mradi huu ambao Serikali imewekeza fedha nyingi tuulinde kama mboni ya jicho. Ukiona mtu anakuja kuhujumu huyo hatutakii mema. Sitarajii na sitegemei kuona watu wanaunganishiwa maji kijanja janja mpaka atoe hela kiasi fulani hapana. Mtu ameomba kuanganishiwa maji ndani ya siku 7 aunganishiwe maji." Amesema Waziri Aweso.

" Ndugu zetu wasoma mita, ni marufuku kumbambikizia Mwananchi bili ya maji. Tunakwenda kubadili uelekeo juu ya Usomaji wa Mita. Tunaenda kuwa na mita za Luku ya maji. Ni marufuku kumkatia mtu yoyote maji siku ya sikukuu na Weekend". Ameongeza Aweso.
View attachment 3275119
Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Mkama Bwire, amemwambia Waziri Aweso kwamba kukamilika kwa Mradi huu kunaenda kumaliza na kupunguza tatizo la Maji katika eneo la Kisarawe(kata ya Kiluvya) na Majimbo matano ya Mkoa wa Dar Es Salaam ikiwemo Jimbo la Ukonga(Kitunda, Kipunguni na Kata ya Mzinga), Jimbo Segerea(Kinyerezi, Bonyokwa pamoja na Segerea), Jimbo la Ubungo(Kata ya Msigani pamoja na Saranga) Jimbo la Temeke(Kaya ya Buza, Yombo pamoja na kata ya Makangarawe).

"Kwa sasa hivi tupo kwenye Majaribio kuhakikisha kwamba wananchi sasa Wanapata maji ya uhakika. Tunaendelea na Majaribio haya ndani ya mwezi huu wa tatu hadi kufikia mwezi wa Nne. Wakati tunafanya majaribio Wananchi wanaendelea kupata maji." amesema Mhandisi Bwire

Mradi wa maji Bangulo umetekelezwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 36 huku ukihusisha kazi za Ujenzi wa Tenki lenye ujazo wa lita milioni 9, Kituo cha Kusukuma Maji na Ulazaji wa bomba kwa umbali wa kilomita 119 na utahudumia wakazi wapatao 450,000 katika Kata za Mzinga, Kipunguni, Kitunda, Pugu station, Kiluvya, Msigani na Kinyerezi.

======

WAZIRI AWESO -SITARAJII WATU KUUGANISHIWA MAJI YA BANGULO KIJANJAJANJA

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameitaka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuwaunganishia maji wananchi watakaonufaika na Mradi wa Maji wa Bangulo kwa ufanisi na uaminifu na kuhakikisha hakuna mianya yoyote ya rushwa itakayojitokeza kwani kuunganishiwa maji ni haki ya msingi ya mwananchi.

Waziri Aweso ameyasema hayo leo Jumanne Machi 18, 2025 alipotembelea mradi huo uliopo mtaa wa Bangulo hali ya hewa katika kata ya Pugu Station wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, ukitazamiwa kunufaisha wananchi 450000 wa kata mbalimbali za wilaya hiyo na wilaya jirani.

"Sitarajii na sitegemei kuona watu wanaunganishiwa maji kijanjajanja mpaka atoe hela kiasi fulani ndiyo aunganishwe, hapana. Mtu ameomba kuunganishiwa maji, DAWASA ninaomba niwaeleze, ndani ya siku saba lazima mtu aunganishiwe maji," amesema Waziri Aweso.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri amewaomba wananchi wa Bangulo kutunza vyema miundombinu ya maji katika eneo lao na kutoa taarifa watakapoona kuna dalili ya kuvuja kwa maji kutokana na baadhi ya mabomba katika eneo hilo kuwa ya muda mrefu. Amesema kwa kufanya hivyo, upotevu wa maji utadhibitiwa na huduma kwa wananchi itaendelea kutolewa kwa ufanisi.

Naye Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Mkama amesema mradi huo umegharimu jumla ya fedha za Kitanzania Shilingu bilioni 36.8 hii inajumuisha gharama ya ujenzi pamoja na usimamizi wa mradi ambapo kwa ujenzi pekee gharama ni Shilingi bilioni 35.0 na usimamizi wa mradi gharama ni Shilingi bilioni 1.8.

Amesema Dar es Salaam upande wa Kusini kulikuwa na changamoto ya maji kutokana na miundo ya kijiografia ya milima lakini kwa mradi huu, wananchi hawatapata shida tena kwani tayari kuna mitandao ya zamani ya maji katika eneo hilo ambayo inaendelea kuboreshwa na kutawekwa mtandao mpya.

Mradi huu unahusisha Manispaa za Ubungo, Temeke, na Jiji la Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma ya maji katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji ukilenga kunufaisha wananchi 450000 wa kata wilayani Ilala za Mzinga, Kipunguni, Kitunda, Pugu station na Kiluvya huku kata za Msigani wilayani Ubungo na Kinyerezi wilayani Ilala zikienda kuongezewa msukumo wa maji.
View attachment 3275060View attachment 3275061View attachment 3275063View attachment 3275064View attachment 3275065View attachment 3275066
Tangi halizalishi maji, maji hujazwa kwenye tangi.
 
Back
Top Bottom