KERO DSM DAWASA mgao, umeme mgao mtatuua Dar jamani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Hiyo inaitwa Samia style.

Mama anauchapa mwingi!
IMG_20250208_151540.jpg
 
Kuzagamua kwenye joto hamna ata raha mnakua kama mko sauna, watupumzishe lasiivyo tutasitisha kuzalisha nguvu kazi ya taifa la kesho. Hili nalo wakalitizame.
 
CCM kama imeshindwa kulifanya tatizo la maji Historia unafikiri nini wanaweza sasa?..

Kama jiji la Dar es salaam halina maji na Rais ndio akaishi, mawaziri wote wanaishi hapo, Tiss director anaishi hapo, CDF anaishi hapo nk unafikiri wapi sasa kutakuwa hakuna shida ya maji?..

Zipo wilaya na miji mikoani huko maisha yao ni maji ya visima huku tukiwa Karne ya 21.
Yaani toka Uhuru 1961 mpaka leo hatuna maji tena kwenye mji mkuu kibiashara, maji ambayo ni basic tumeshindwa unafikiri tunaweza nini sasa?
 
Ni wakati sasa wakuiadhibu CCM na mawakala wao bongo movie, bongo fleva na machawa wote ili heshima ya Taifa irudi.

Taifa linahitaji ukombozi kutoka kwenye mikono ya mkoloni CCM ili hizi shida zote ambazo ni basic ziishe.

Viongozi wanapataje nguvu yakutembelea magari ya kifahari na misafara mirefu ilihali Taifa limeshindwa kutatua shida za msingi kama maji, umeme, miundombinu, Elimu na Afya? Raha iko wapi kama basics tu zinatushinda?

Ziara zinatumia mamilioni ya hela ambazo zingeweza kuondoa kero nyingi sana za msingi.
 
Na hili jua huku unapigwa mgao wa maji wiki nzima , ukirudi japo uwashe feni unapigwa mgao wa umeme basi unakaa kama mbuzi mwenye kiu ukibweka huku ulimi nje ......mtatuua jamani ..... achilieni hata maji tu
Na bado ndani ya miaka hii 10 mpaka maji muite mma
 
Na hili jua huku unapigwa mgao wa maji wiki nzima , ukirudi japo uwashe feni unapigwa mgao wa umeme basi unakaa kama mbuzi mwenye kiu ukibweka huku ulimi nje ......mtatuua jamani ..... achilieni hata maji tu
Hakuna Mji wa hovyo kuishi kama Dar

Huko Hadi hewa safi ni ya mgao 😆😆

My Take
Mkiambiwa lipeni tozo Serikali ilete Huduma Huwa mnapinga na mnalalmika sana.

Bado hamjasema Hadi mseme yaani ndio kwanza bwawa la kidunda Liko.20% 😂😂
 
Back
Top Bottom