Dawa asilia sasa kuwekewa mkakati wa kupatikana katika Vituo vya kutolea Huduma za Afya na Maduka ya Dawa za Binadamu

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
126
Na WAMJW - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeweka mkakati wa kusogeza karibu huduma za tiba asili kwa jamii ambazo sasa dawa hizo asilia zinawekewa mikakati ya kupatikana hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na maduka ya kuuza dawa za binadamu.

Hayo yamesewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mara baada ya kufanya kikao na wazalishaji wa dawa hizo asilia nchini ambao dawa zao zimethibitishwa Usalama na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Msajili wa Tiba Asili nchini na kukidhi vigezo vya kutumika kwa binadamu.

“Sisi watendaji tumeona ni muhimu kukutana ili tuweze kuweka mikakati ya kuhakikisha hizi dawa asili zinawafikia wananchini kwa urahisi zaidi”amesema Prof. Makubi.

Amesema kuwa tunasumbuliwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza hivyo ni lazima tutumie silaha (dawa asilia na za kisasa) zote ambazo ni salama zinaweza kusaidia wananchi kwa afya.

“Kuna hizi dawa asili zenye usalama, ambazo zimekuwa zikitumika kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambikiza hivyo ni lazima tuzisogeze karibu kwa wananchi kupitia mawakala, maduka ya madawa ya binadamu nata hospitalini kwa usalama ziweze kuwafikia wananchi” ameeleza Prof. Makubi.

Aidha Prof. Makubi amewataka wasomi na wataalam wa afya kwa ujumla kubadili mtazamo wao juu ya tiba asili kwa kuwa zimekuwa na mchango mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na kuwaasa wataalam kutokuwa kikwazo kwa wananchi kutumia tiba asili.

“Kama dawa sisi tumeshaihakiki na tukaikubali kwamba hii dawa ni salama, basi pasiwepo na kinyongo au ugumu wowote wa sisi watumishi wa afya kuruhusu mwananchi kutibiwa kwa dawa hiyo ”Amesisitiza Prof. Makubi.

Katika hatua nyingine Prof. Makubi hakusita kuwaasa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kinga za magonjwa magonjwa yote ikiwemo kufanya mazoezi, kubadili mtindo wa maisha na kula chakula bora. Wananchi siyo lazima wasubiri matamko ya Serikali katika kujikinga na magonjwa; njia nyingi za kujikinga na magonjwa zimeshatolewa na wanazijua; kwa hiyo ni suala la wao kujenga mazoea ya kujikinga kila siku ya Mungu.

Prof Makubi alielezea pia umuhimu wa kufanya tafiti zaidi katika tiba asilia ili ziweze kuhakikia kwa miongozo ya nchi na kimataifa na baadae kuweza hata kuhudumia wananchi wa nchi za jirani. Aidha alisisitiza kuwa Wagunduzi watalindwa na Serikali na kuhakikisha umiliki wa ugunduzi wa dawa hizo haupotei wakati na baada ya utafiti.

Naye Dkt. Paul Mhame, Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa Serikali kupitia Taasisi zake imeweza kuchambua na kuidhinisha dawa za kunywa aina 5 na dawa aina 4 za mafuta tete kwa ajili ya kujifukiza ambazo zimekidhidi vigezo kuweza kutumika kwa binadamu. Amezitaja dawa hizo za kunywa kuwa ni NIMRICAF, COVIDOL, BINGWA, PLANET ++ pamoja na COVOTANZA huku zile za mafuta tete zikiwa ni BUPIJI pamoja na UZIMA.

“Aidha Serikali inaendelea kufanya kazi kwa karibu na wazalishaji wengine ambao wakikidhi vigezo dawa zao zitaongezwa kwenye orodha hii” Amesema Dkt. Mhame na kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kununua dawa hizo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ambukizi na yasiyoambukiza.

Akizungumuza kwa niaba ya wazalishaji wa dawa asili Bw. George Buchafwe ambaye ametengeneza dawa ya kujifukiza kwa mafuta tete ya Bupiji ameishukuru Serikali kwa kuona mchango wao na kuwa sehemu ya kuchangia na kuboresha afya za wananchi.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutambua kuwawapo watafiti ambao wanaweza wakaisaidia jamii yetu na ikawezakutoka katika hatua kwenda hatua nyingine kwa kutumia tiba zetu za asili” Amesema Bw. Buchafwe.

Amesema kuwa wao wazalishaji wa dawa za asili wapo tayari kushirikiana na Serikali kuzalisha bidhaa bora ye usalama kwa afya ya binadamu.

Kwa upande wake Dr Otieno kutoka Taasisi ya Tiba Asilia Muhimbili amesisitiza umuhimu wa wananchi kuacha kuchanganya dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja wakati wa kutumia. Amesema ni vema pia wananchi wafuate maelekezo sahihi ya matumizi ya hizi dawa na kuzingatia usalama wake.

Tatizo buraa buraa nyingi
.
Dawa yoyote ile lazima pharmacokinetics , pharmacodynamics, body distribution yake, half-life yake possible adverse effects , interactions and the likes zifahamike Kwanza tena kwa tafti zisizo nashaka.sasa kuzipigia mapambio tu bila kuainisha vitu Kama hivi kwenye hizi juice zetu.ni kazi bure.

Sipingi Wala kukejeli uwezo wa hizi dawa but nivizuri vitu Kama hivyo viainishwe.
na vipi kuhusu approval ya TMDA?

Tusiburuzane tu Kisa mkulu kasema.
 
Life span ya
1. Wajapan
2. Wachina
3. Bhutan
4. Wahindi
Ilipanda baada ya Kuthamini na Kutambua mchango wa Tiba za Asili
Hongera prof. Abel Makubi
Naomba utizame pia yafuatayo,
  1. Uadilifu wa watu uliowataja
  2. Imani ya watu uliowataja
Kwa sisi ambao tuko tayari kukaanga chips kwa mafuta ya transfoma ili tupate pesa, aahhhhhhhhhhhhhhhhh

Kibali cha mkemia mkuu ndicho kinatumika kuaminisha watu kuwa dawa inatibu. Leo tuna matapeli wanapita na vi pc wakitangaza kuwa wanapima mwili mzima kwa 15000, utapeli mkubwa na serikali iko kimya.
 
Tunashukuru kwa Taarifa hii. Dawa hizi kwa Sasa zinapatikana wapi?? Kwa tulioko vijijini tunazipataje??
 
Nchi zilizoendelea kwenye Sekta ya dawa kama Marekani, India na China tiba asili inaendelezwa sana na kuwekezewa fedha nyingi sana. Sisi huku Afrika wamishionary walituambia dawa [na hata majina] yetu kuwa ni ya kipagan.

Ni vyema kama sasa tunaamka. Muhimu tu kuwekeza vya kutosha kwenye tafiti. Hakuna dawa mwanadamu wa sasa ataiamini bila kufanyiwa utafiti wa kutosha.
 
Ninyi mmeamua kuua watanzania, inawezekana mzigo wa kulipa pensheni umekua mkubwa baada ya serikali kukwapua fedha kutoka kwenye mifuko ya hifadhi za jamii. Sasa mmekuja na mkakati wa kuua wazee wetu.
 
Tutumai na kuomba aishie hapo. Wasiwasi wangu kuwa wasije wakatushauri oia tutumie mahabara na vipimo vya waganga wa asili.

Wakati tunatumia madawa hayo tujiandae pia kwa madhara yake ya muda mrefu.

Hakika utamaduni unadumu hata ukibafilika vipi!
 
Kwa hiyo wasomi wa Tanzania ndio tumefikia hapa, mtaanza ku-prescribe dawa ambazo hazina pharmacological data kwa wagonjwa. Msije mkaleta shida nyingine ya magonjwa ya figo na ini...
masai anakula nyama sana haugui sababu ya dawa za kimasai zikipelekwa kupimwa kwenye kipimo mzungu hicho kipimo mzung kitakataa kuitabua sababu kimekuwa programmed ku accept vya kizungu tu

Nashauri kama ilivyo kwa wahindi na wachina tuanzishe vyuo vyetu vya kufundisha Traditional Medicine kuanzia certificate hadi Phd .China na India ziko hadi Phd n Traditional medicines kuua huu ukoloni wa kusomea tu degree za wazungu za TIba hongereni wizara ya afya

hili pia litainua uchumi wa nchi na kuongeza kipato kwa wazalishaji wa dawa asilia na itaokoa pesa nyingi za kigeni

mimi pia nina dawa yangu ya ugonjwa fulani nitaingia uzalishaji mkubwa
 
Yaani hii yote ni kutokumkwanza mkuu...anyway hata dawa za arv tuache tu
 
Tunashukuru kwa Taarifa hii. Dawa hizi kwa Sasa zinapatikana wapi?? Kwa tulioko vijijini tunazipataje??
Ebo dawa hizo zimetokea vijijini hukohuko. Sawa za mijini zimeonekana kushindwa kuhimili varangati lanshambulizi la COVID 19. Hii ni Kwa mujibu wa maprofesa wa Magufuli!
 
Huyu jamaa asipoondolewa madarakani mapema ataliangamiza taifa walahi!
 
Na WAMJW - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeweka mkakati wa kusogeza karibu huduma za tiba asili kwa jamii ambazo sasa dawa hizo asilia zinawekewa mikakati ya kupatikana hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na maduka ya kuuza dawa za binadamu.

Hayo yamesewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi mara baada ya kufanya kikao na wazalishaji wa dawa hizo asilia nchini ambao dawa zao zimethibitishwa Usalama na Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na Msajili wa Tiba Asili nchini na kukidhi vigezo vya kutumika kwa binadamu.

“Sisi watendaji tumeona ni muhimu kukutana ili tuweze kuweka mikakati ya kuhakikisha hizi dawa asili zinawafikia wananchini kwa urahisi zaidi”amesema Prof. Makubi.

Amesema kuwa tunasumbuliwa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza hivyo ni lazima tutumie silaha (dawa asilia na za kisasa) zote ambazo ni salama zinaweza kusaidia wananchi kwa afya.

“Kuna hizi dawa asili zenye usalama, ambazo zimekuwa zikitumika kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambikiza hivyo ni lazima tuzisogeze karibu kwa wananchi kupitia mawakala, maduka ya madawa ya binadamu nata hospitalini kwa usalama ziweze kuwafikia wananchi” ameeleza Prof. Makubi.

Aidha Prof. Makubi amewataka wasomi na wataalam wa afya kwa ujumla kubadili mtazamo wao juu ya tiba asili kwa kuwa zimekuwa na mchango mkubwa wa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na kuwaasa wataalam kutokuwa kikwazo kwa wananchi kutumia tiba asili.

“Kama dawa sisi tumeshaihakiki na tukaikubali kwamba hii dawa ni salama, basi pasiwepo na kinyongo au ugumu wowote wa sisi watumishi wa afya kuruhusu mwananchi kutibiwa kwa dawa hiyo ”Amesisitiza Prof. Makubi.

Katika hatua nyingine Prof. Makubi hakusita kuwaasa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za kinga za magonjwa magonjwa yote ikiwemo kufanya mazoezi, kubadili mtindo wa maisha na kula chakula bora. Wananchi siyo lazima wasubiri matamko ya Serikali katika kujikinga na magonjwa; njia nyingi za kujikinga na magonjwa zimeshatolewa na wanazijua; kwa hiyo ni suala la wao kujenga mazoea ya kujikinga kila siku ya Mungu.

Prof Makubi alielezea pia umuhimu wa kufanya tafiti zaidi katika tiba asilia ili ziweze kuhakikia kwa miongozo ya nchi na kimataifa na baadae kuweza hata kuhudumia wananchi wa nchi za jirani. Aidha alisisitiza kuwa Wagunduzi watalindwa na Serikali na kuhakikisha umiliki wa ugunduzi wa dawa hizo haupotei wakati na baada ya utafiti.

Naye Dkt. Paul Mhame, Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa Serikali kupitia Taasisi zake imeweza kuchambua na kuidhinisha dawa za kunywa aina 5 na dawa aina 4 za mafuta tete kwa ajili ya kujifukiza ambazo zimekidhidi vigezo kuweza kutumika kwa binadamu. Amezitaja dawa hizo za kunywa kuwa ni NIMRICAF, COVIDOL, BINGWA, PLANET ++ pamoja na COVOTANZA huku zile za mafuta tete zikiwa ni BUPIJI pamoja na UZIMA.

“Aidha Serikali inaendelea kufanya kazi kwa karibu na wazalishaji wengine ambao wakikidhi vigezo dawa zao zitaongezwa kwenye orodha hii” Amesema Dkt. Mhame na kuwasisitiza wananchi kujitokeza kwenda kununua dawa hizo kwa ajili ya kujikinga na magonjwa ambukizi na yasiyoambukiza.

Akizungumuza kwa niaba ya wazalishaji wa dawa asili Bw. George Buchafwe ambaye ametengeneza dawa ya kujifukiza kwa mafuta tete ya Bupiji ameishukuru Serikali kwa kuona mchango wao na kuwa sehemu ya kuchangia na kuboresha afya za wananchi.

“Tunaishukuru Serikali kwa kutambua kuwawapo watafiti ambao wanaweza wakaisaidia jamii yetu na ikawezakutoka katika hatua kwenda hatua nyingine kwa kutumia tiba zetu za asili” Amesema Bw. Buchafwe.

Amesema kuwa wao wazalishaji wa dawa za asili wapo tayari kushirikiana na Serikali kuzalisha bidhaa bora ye usalama kwa afya ya binadamu.

Kwa upande wake Dr Otieno kutoka Taasisi ya Tiba Asilia Muhimbili amesisitiza umuhimu wa wananchi kuacha kuchanganya dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja wakati wa kutumia. Amesema ni vema pia wananchi wafuate maelekezo sahihi ya matumizi ya hizi dawa na kuzingatia usalama wake.

Yaani mtaala wote aliosomea huyu Chief Medical Officer ni tiba ya kisasa na ndiyo mtaala huo huo aliofundishia mpaka akawa Process.

Leo anausaliti kwa ajili ya kumfurahisha Meko? Napendekeza Prof Makubi nanwenzie warudishe vyeti kwenye vyuo walivyosoma. Huu ni UWENDAWAZIMU
 
Back
Top Bottom