BAADA YA JECHA KUMTANGAZA DR SHEIN KUWA RAIS WA ZANZIBAR, MTATIRO AANDIKA HIVI KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK DAKIKA CHACHE ZILIZOPITA
FAKING NEWS: SHEIN ASHINDA KWA KISHINDO!!!!!!
Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Shein ametangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais cha Zanzibar katika uchaguzi ambao ulikuwa na ushindani mkali kuwahi kutokea katika historia ya Zanzibar.
Dk. Shein amepigiwa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4 akifuatiwa na mpinzani wake mkuu na mwanasiasa machachari, Hamad Rashid Mohamed wa ADC aliyepata kura 9,734 sawa na asilimia 3.0.
MY TAKE;
Haya ni maajabu ya dunia, sijui tuyape namba ngapi! Yani kura upige mwenyewe, uzihesabu mwenyewe, ujitangaze mwenyewe na kisha unataka tushangilie wote.
Hata hivyo hatuna budi kutoa pongezi na hongera kwa CCM, Dk. Shein, Mazombi wote, watekaji wote na wale wote wanaowashikilia kina Mansour gerezani! Mungu atawalipa sawa sawa na kwa kipimo kile kile lakini kubwa kuliko yote, watanzania na hata wazanzibari wanakomazwa na wanafundishwa kuwachukia kutoka mioyoni mwao, madhara yake huonekana baada ya muda, ni kama HIV na UKIMWI.
Ni kweli kabisa kuwa #Nchi_Ya_Kimapunduzi_Haitolewi_Kwa_Kura_Wala_Uchaguzi!
Ongozeni hadi mwisho wa dahari.
Mtatiro J.