Darasa la nyumbani (private learning)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,719
215,811
Kuna utaratibu nimeugundua katika nchi za magharibi kuwa mazai anao uwezo wa kuajiri mwalimu wa kumfundisha mtoto/watoto wake nyumbani kama hataki watoto hao waende shuleni kama watoto wengine. Mazazi anatakiwa kwenda kwenye ofisi ya elimu na kueleza nia yake, watampa msaada jinsi ya kupata mwalimu, mradi mwalimu awe na vigezo vya kutoa elimu stahiki, na syllabus itafuatwa ya taifa. Mwalimu huyu anakaguliwa kila baada ya term na watoto wanaandikishwa kufanya mtihani wa taifa kwenye kituo cha karibu na unapokaa.

Serikali inalipa mshahara wa mwalimu iwapo mwanafunzi hawezi kuhudhuria darasa katika shule ya kawaida kwa sababu za kiafya, magonjwa kama leukaemia ambapo mtoto anakua na low immune au immune suppress. Watoto wengine ni kwa utukutu uliopitiliza, na kila akiwa darasani anapiga watoto wenzake, kwakua ni sheria kila mtoto apate elimu, serikali inaweza kugharamia mshahara wa mwalimi.

Kuna wale wazazi ambao wanapenda wenyewe watoto wao wasijichanye na watoto wengine, wanaamua kulipa mshahara wa mwalimu na watoto wanafundishwa nyumbani.

Kama una uwezo huo ungependelea mtoto wako afundishwe nyumbani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…