Dar yaendelea kuongoza kwa Wateja wa Huduma za Mawasiliano Tanzania, ina Wateja Milioni 12.9

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,817
1706511681271.png

Ripoti ya Robo ya Mwisho wa Mwaka 2023 inayoangazia Huduma za Mawasiliano Nchini, imeonesha hadi kufikia Desemba 2023, jumla ya Wateja 70,290,876 wa Huduma za Mawasiliano walisajiliwa, ikiwa ni ongezeko la 4.7% kutoka Wateja Milioni 67.1 waliokuwepo Septemba 2023.

Mkoa wa Dar es Salaam umeongoza kwa idadi kubwa ya Usajili wa Huduma za Mawasiliano ikiwa na Wateja Milioni 12.9 (18.4%). Mwanza unafuatia ukiwa na 6.6%, Arusha 6.0%, Mbeya 5.8%, Dodoma 5.3%. Mikoa ya yenye Wateja chini ya 100,000 kila mmoja ni Kusini Unguja na Kaskazini Unguja.

Mtandao wa Vodacom umefikisha Wateja 21,272,484 (30%) ukifuatiwa na tiGO wenye Wateja 19,698,263 (28%), Airtel 19,146,016 27%, Halotel 8,529,919 (12%) na TTCL 1,644,194 (3%).
1706511705190.png

1706511730643.png
 
Nape hapo anapiga hela ndefu sana kila mwezi. Na sasa hivi alivyombania Elon musk. Nape ni trilionea.

Wizara ya kina Mwana FA hamna upigaji kabisa. Labda wapige panga kwenye vijisafari uchwara ya viconcert uchwara.
 
Wananchi million 4 line za simu million12 kwel dar matapeli ni weng sana
Hao wananch milion4 kuna watoto vichaa matahila ambao hawawezi miliki line
 
Nimeona ile list,
Toka 2021 wateja wanaongezeka kwa speed sana sijui ni nzuri au mbaya,
 
Back
Top Bottom