BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,803
Vijana wawili, Erick Filbert (27) na Jafari Said (23) wakazi wa Wilaya ya Temeke wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa mashtaka ya ubakaji.
Wawili hao wamesomewa mashtaka yao wanayodaiwa kuyatenda kwa nyakati tofauti na Wakili wa Serikali, Amedeus Mallya mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Ajali Milanzi.
Mshtakiwa Erick Filbert anakabiliwa na makosa mawili, kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma Shule ya Sekondari Taifa, kinyume na kifungu cha 130, (1) (2e) na 131 (1) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 marejeo ya mwaka 2022.
Shtaka la pili ni kumpa ujauzito mwanafunzi huyo kinyume na kifungu 60A (3) cha Sheria ya Elimu namba 353 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016.
Akisoma shtaka dhidi ya Jafari Said, wakili Mallya amesema, "Mtuhumiwa alifanya mapenzi bila ridhaa na binti wa miaka 18 mnamo Agosti 12, 2023 eneo la Saku Ilulu wilayani Temeke kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu namba 16 kifungu cha 130 (1) (2a) na 131 (1) marejeo ya mwaka 2022."
Washtakiwa wote wamekana makosa yao na kuachiwa kwa dhamana, mashauri yao yatasikilizwa tena Septemba 20, 2023.
MWANANCHI