Dar: Wasichana wawili wa miaka 16 na 12 wajiteka ili kudai pesa kutoka kwa Wazazi wao

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
794
1,676
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewashikili na kuwahoji Wasichana wawili kutoka Vijibweni, Kigamboni wenye umri wa miaka 16 na 12, kwa madai ya kutengeneza mazingira ya kujiteka ili kudai pesa kutoka kwa Wazazi wao ambapo Uchunguzi umebaini kuwa walitoweka kwa siku mbili na kulala ufukweni kabla ya kuendelea kujificha maeneo ya Tungi hadi walipokamatwa.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa Watoto hao walikiri kupanga njama hiyo kwa lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kitendo hicho ni kosa la jinai na limeonya Wananchi dhidi ya upotoshaji wa taarifa za usalama.

 
Wazazi pendeni watoto wenu na muwape mahitaji ya muhimu haya hayatatokea.

Kama huwezi kulea mtoto na kumpatia mahitaji yake yotw usizae.
 
Back
Top Bottom