BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,810
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule amesema Mvua zilizonyesha Novemba 12, 2023 zimesababisha uharibufu kwenye nyumba takriban 500 katika eneo la Kigogo kutokana na Maji kujaa kwenye Mto Msimbazi.
DC Mtambule amesema, nyumba za eneo hilo zimezingirwa na kiasi kikubwa cha Maji ambapo kwa sasa jitihada Mamlaka za Uokoaji ikiwemo Jeshi la Zimamoto ziko eneo la tukio kwaajili ya kushughulikia suala hilo.
Pia, Mvua hizo zilizonyesha kwa zaidi ya saa 10 katika maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam zimesababisha madhara kwenye Miundombinu muhimu ikiwa pamoja na Shule ya Msingi Michael Urio ambayo imezingirwa na Maji.