Dar: Mussa Khamis Bakari aka Buda, akamatwa kwa kumuua rafiki yake Abdallah Twahir Selemani kisha kumpora Milioni 61

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,093
13,933
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kusimamia mkakati wake maalum wa kuzuia vitendo vyote vya kihalifu katika jiji la Dar es Salaam. Tarehe 28 Juni 2024 lilimkamata na kumuhoji kwa kina Mussa Khamis Bakari buda (30) wakala wa Forodha, Mkazi wa Temeke kwa tuhuma za mauaji ya Abdallah Twahir Selemani ambaye alikuwa rafiki yake na baada ya kumuua alifanikiwa kuiiba pesa za marehemu Tsh Milioni 61 kutoka kwenye akaunti ya huyo rafiki yake.
Taarifa fupi za tukio ni kuwa tarehe 1 Mei, 2024 majira ya saa 10:20 asubuhi huko maeneo Mbutu Kichangani, Kigamboni pembezoni mwa barabara itokayo Cheka kuelekea beach ya Kichangani uliokotwa mwili wa mtu mmoja mwanaume akiwa ameshafariki na baadae mwili huo ulitambuliwa kuwa ni Abdallah Twahir Selemani mkazi wa Chanika.

Awali tarehe 4 Mei 2024 Jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kupotea kwa Abulllah Twahir Selemani kutoka kwa mama yake kuwa alipotea katika mazingira ya kutatanisha. Uchunguzi wa Jeshi la Polisi baadae uligundua kuwa tarehe 30 Aprili 2024 mtuhumiwa Mussa Khamis Bakari buda alikuwa na marehemu wakitumia gari namba T.928 DFY Suzuki Kei wakitokea Magomeni kuelekea Temeke, Kijichi mpaka eneo ulipokutwa mwili wa marehemu.

Uchunguzi wa vitu mbalimbali umebainisha mtuhumiwa alimuua na baadae kwenda kutupa mwili huo pembezoni mwa barabara ulipookotwa .

Baada ya kumuua, mtuhumiwa alichukua kadi ya benki ya marehemu na kwa nyakati tofauti tofauti alianza kutoa pesa kiasi cha shilingi Milioni 61 kutoka kwenye akaunti ya marehemu. Chanzo cha mauaji ni tamaa ya kutaka kuiba pesa kutoka kwa rafiki yake ambaye sasa ni marehemu. Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi limefuatilia matukio ya unyan’ganyi na wizi wa pikipiki katika Jiji la Dar es Salaam na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 23 na pikipiki 39 zilizoibwa maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

Watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia mbinu ya kujifanya abiria na wakifika njiani hujitokeza watu wengine ambao humtishia dereva kwa mapanga kumjeruhi na kumuibia pikipiki hiyo, wakatii mwingine pikipiki zinazokuwa zimeegeshwa nje hutumia mbinu ya kuunganisha waya, kuwasha na kuiba pikipiki hizo.

Ufuatiliaji wa Jeshil la Polisi umebaini watuhumiwa hao baada ya kuziiba pikipiki wamekuwa wakiziuza kwa gharama nafuu mikoa mbalimbali ikiwemo Mikoa ya Dodoma na Singida.

Ufutiliaji huo umefakiwa kukamata risiti za kugushi 18 za kusafirishia pikipiki za wizi, kadi 11 za usajili wa pikipiki za kugushi, kadi (03) za usajili wa magari za kugushi, vyeti mbalimbali vya kuzaliwa na kimoja cha ndoa vya kugushi, plate number (03) za pikipiki, kitabu kimoja cha bima ya magari, nyaraka mbalimbali za TRA, barua mbalimbali zenye nembo za jeshi la Polisi Tanzania, mihuri mbalimbali ya manispaa ya Kinondoni,Temeke, IIala, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, RITA, Mamlaka ya Bandari na mhuri mmoja wa moto ulioandikwa "United Republic of Tanzania" wenye nembo ya bibi na bwana, leaf 56 za kutengenezea kadi za vyombo vya moto, leaf 86 za kutengenezea vyeti vya vizazi na vifo vyenye nembo ya msajili wa vizazi na vifo.

Wakati huo huo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linakanusha taarifa ya sauti inayosambaaa kwenye mitandao ya kijamii ikielezea kuwepo kwa tukio la mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kutekwa nyara maeneo ya kituo cha kontena kilichopo ndani ya chuo hicho na watu wasiojulikana wakitumia usafiri wa bajaji kisha kupelekwa Kimara na baadae kutelekezwa eneo la Masaki.
Jeshi la Polisi limefanya ufuatiliaji wa taarifa hiyo na kubaini kuwa ujumbe huo wa sauti ni wa muda mrefu zaidi ya miaka mitano nyuma na uliwahi kusambazwa kama ulivyo na ufuatiliaji wake ulifanyika ikabainika kuwa hazikuwa habari za kweli .

Polisi wamebaini pia tukio lililoelezwa kuwa kuna mtu aliuawa Sinza kisha kuondolewa ziwa upande wa kushoto na sehemu za siri, hazikuwa habari za kweli na hakuna tukio la namna hiyo kama linavyoelezwa.

Kuzusha taarifa za uongo zenye lengo la kujenga taharuki au hofu ni makosa.Tunatahadharisha juu ya tabia hizo na Jeshi halitasita kuwatafuta na kuwahoji wanaohusika kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam pia katika kusimamia mifumo ya kisheria ya haki jinai limeendelea kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya kihalifu na hatimaye kupatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu. Jeshi la Polisi limekuwa likichukizwa sana na vitendo vya ubakaji na ulawiti na katika hatua hiyo mwaka 2023 Juni, mshtakiwa Hussein Shomvi (50) fundi ujenzi, mkazi wa Chanika Zogoali alikamatwa na baadae kufikishwa Mahakama ya Kinyerezi na baada ya mashauri yake kusikilizwa tarehe 10 Juni 2024 alipatikana na hatia ya kosa kulawiti watoto wawili wa kiume wa shule ya msingi na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Washtakiwa wengine Shamim Hamadi @dj mush (30) Mkazi wa Kimara Mwisho, na Waziri Ramadhani (26) Mkazi wa Mbezi Luis na Seif Salum (19) mkazi wa Manzese wote kwa pamoja mwaka 2022 walifikishwa Mahakama ya Kinondoni mbele ya Hakimu Mkazi Nabwike Mbaba na baada ya mashauri yao kusikilizwa terehe 10 Juni 2024 walipatikana na hatia ya Unyangayi wa kutumia silaha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali, zitatunzwa na wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi
Dar es Salaam
IMG-20240711-WA0016.jpg
IMG-20240711-WA0018.jpg
IMG-20240711-WA0014.jpg
 
View attachment 3039367View attachment 3039368View attachment 3039369
Okay sawa. Taarifa nzuri ingawaje kuna walakini juu ya ukweli au usahihi wake.

Ombi kwa Wale watu wenye accessibility na mfumo wa usajili wa Wamiliki wa magari Tz, watusaidie kumfahamu Mmiliki wa gari hilo lenye Namba ya T928 DFY. Nani Mmiliki wa gari hili?

Je, hizo pesa Tshs. 61 Milioni zilizoibiwa zilitolewa kutoka kwenye Bank Account moja tu ya marehemu au kutoka kwenye akaunti tofauti tofauti za benki? Kama pesa kiasi kikubwa namna hiyo kilitolewa na huyo Mtuhumiwa wa Mauaji kutoka kwenye akaunti moja tu ya Benki, Je, kwa nini Jeshi la Polisi halikuweza kuingilia haraka sana mawasiliano ya ki-electronic ya marehemu sambamba na kuingilia haraka sana miamala ya fedha ya kwenye akaunti za benki za marehemu huyo Mara tu baada ya Mama wa marehemu kuripoti taarifa ya kupotea kwa mwanaye katika Jeshi hilo?????? Kwa nini Jeshi la Polisi halikuchukua hatua za haraka za kuingilia mawasiliano ya ki-electronic ya marehemu sambamba na kwenda kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na masuala ya kibenki ya akaunti za mtu ambaye Jeshi hilo lilipewa taarifa rasmi juu ya kupotea kwake katika Mazingira ya kutatanisha???Kulikoni Jeshi hilo lilikaa kimya kabisa kiasi Cha kusababisha kiasi kikubwa Cha fedha kutolewa kutoka kwenye akaunti ya benki ya huyo marehemu ambaye mapema kabisa Jeshi la Polisi lilipatiwa taarifa za kupotea kwake?????????
Kwa sababu kwa mujibu wa taratibu za Benki, kiasi kikubwa cha fedha (i.e Tshs 61 Milioni) hakiwezi kutolewa kwa mkupuo mmoja tu kutoka kwenye Benki bila ya Benki husika kupewa taarifa za awali kwanza za kuwepo kwa muamala wa namna hiyo.
Are they (Police Force) an accessory for the crime????

Uchunguzi wa kina kabisa ulio huru unahitajika Sana kwenye mkasa huu ili ukweli halisi ujulikane.

Narudia Tena kuwaasa Jeshi la Polisi, tambueni kwamba ni kweli kuwa Tanzania wapo watu wajinga wengi sana, lakini siyo kweli hata kidogo kwamba Watanzania wote kabisa ni Watu wajinga
 
Are they an accessory for the crime????

Aisee, hoja zako za msingi sana.
Password alizitoa wapi wakati wa kutoa hela?
 
Mm nadhani swali hapa ni amepataje password alimtisha marehemu au laah.
Ila usome vizuri, hakutoa kwa mkupuo. Ametoa kidogo kidogo. Mwezi mzima toka mwili uokotwe ndio jamaa kakamatwa. Meaning Huyu alikua akitoa hela mara kwa mara.

Hiyo ni kutokana na upelelezi. Sijui umeniellewa.
 
Hoja yangu ipo hapo hapo kwenye suala la kutoa pesa kidogo kidogo kutoka kwenye Akaunti ya Benki ya marehemu. Je, mtuhumiwa huyo aliwezaje kufanya hivyo bila ya Jeshi la Polisi kumshitukia na kumkamata mapema wakati Jeshi hilo tayari lilishapata taarifa mapema za kupotea kwa mtu ambaye ni Mmiliki wa akaunti ya benki yenye fedha zinazoibiwa????????
Je, wananchi tunawezaje kuamini kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa halishirikiani na huyo Mtuhumiwa katika kuiba fedha za marehemu huko benki?????
Nafikiri umenielewa sasa
 
Okay sawa. Taarifa nzuri ingawaje kuna walakini juu ya ukweli au usahihi wake.

Ombi kwa Wale watu wenye accessibility na mfumo wa usajili wa Wamiliki wa magari Tz, watusaidie kumfahamu Mmiliki wa gari hilo lenye Namba ya T928 DFY. Nani Mmiliki wa gari hili?

Je, hizo pesa Tshs. 61 Milioni zilizoibiwa zilitolewa kutoka kwenye Bank Account moja tu ya marehemu au kutoka kwenye akaunti tofauti tofauti za benki? Kama pesa kiasi kikubwa namna hiyo kilitolewa na huyo Mtuhumiwa wa Mauaji kutoka kwenye akaunti moja tu ya Benki, Je, kwa nini Jeshi la Polisi halikuweza kuingilia haraka sana mawasiliano ya ki-electronic ya marehemu sambamba na kuingilia haraka sana miamala ya fedha ya kwenye akaunti za benki za marehemu huyo Mara tu baada ya Mama wa marehemu kuripoti taarifa ya kupotea kwa mwanaye katika Jeshi hilo?????? Kwa nini Jeshi la Polisi halikuchukua hatua za haraka za kuingilia mawasiliano ya ki-electronic ya marehemu sambamba na kwenda kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na masuala ya kibenki ya akaunti za mtu ambaye Jeshi hilo lilipewa taarifa rasmi juu ya kupotea kwake katika Mazingira ya kutatanisha???Kulikoni Jeshi hilo lilikaa kimya kabisa kiasi Cha kusababisha kiasi kikubwa Cha fedha kutolewa kutoka kwenye akaunti ya benki ya huyo marehemu ambaye mapema kabisa Jeshi la Polisi lilipatiwa taarifa za kupotea kwake?????????
Kwa sababu kwa mujibu wa taratibu za Benki, kiasi kikubwa cha fedha (i.e Tshs 61 Milioni) hakiwezi kutolewa kwa mkupuo mmoja tu kutoka kwenye Benki bila ya Benki husika kupewa taarifa za awali kwanza za kuwepo kwa muamala wa namna hiyo.
Are they (Police Force) an accessory for the crime????

Uchunguzi wa kina kabisa ulio huru unahitajika Sana kwenye mkasa huu ili ukweli halisi ujulikane.

Narudia Tena kuwaasa Jeshi la Polisi, tambueni kwamba ni kweli kuwa Tanzania wapo watu wajinga wengi sana, lakini siyo kweli hata kidogo kwamba Watanzania wote kabisa ni Watu wajinga
Hasa ni ipi hoja yako
 
Hoja yangu ipo hapo hapo kwenye suala la kutoa pesa kidogo kidogo kutoka kwenye Akaunti ya Benki ya marehemu. Je, mtuhumiwa huyo aliwezaje kufanya hivyo bila ya Jeshi la Polisi kumshitukia na kumkamata mapema wakati Jeshi hilo tayari lilishapata taarifa mapema za kupotea kwa mtu ambaye ni Mmiliki wa akaunti ya benki yenye fedha zinazoibiwa????????
Je, wananchi tunawezaje kuamini kwamba Jeshi la Polisi lilikuwa halishirikiani na huyo Mtuhumiwa katika kuiba fedha za marehemu huko benki?????
Nafikiri umenielewa sasa
Bado hujaelewa na unarise ground zako. Soma taarifa vzuri, kuna tarehe za mwili kapatikana.na tarehe za mtuhumiwa kukamatwa
 
Back
Top Bottom