Dar eS salaam: Waziri wa fedha DR Mwigulu Lameck Nchemba ameongoza waombolezaji kifo cha Amani Simbayo

TRA Tanzania

Senior Member
Jul 16, 2022
124
363
WAZIRI NA MTOTO WA MAREHEMU.jpg
WAZIRI NENO.jpg

Waziri wa fedha Dr Mwigulu Lameck Nchemba leo tarehe 8/12/2024 ameongoza waombolezaji na ndugu wa marehemu Amani Simbayo katika kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Malinyi kwa ajili ya mazishi.

Soma Pia:
Katika hotuba yake Mhe Waziri Mwigulu amisisitiza wananchi kutokujichukulia sheria mikononi na kusikitishwa na kitendo kilichopelekea kifo cha Amani.

RC NENO.jpg
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila amekemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi kujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mikoni na kusema kuwa vipo vyombo husika vilivyopewa dhamana ya kusimamia sheria.

CG NA MTOTO.jpg

CG NENO.jpg
Kwa upande wake Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Yusuph Mwenda amewapa pole wafiwa na kusema TRA itaangalia namna ya kumsaidia mjane pamoja na watoto wa marehemu.Amesisitiza kuwa marehemu alikuwa kwenye majukumu yake kwa mujibu wa sheria na ameuwawa akiwa anatekeleza majukumu yake kusimamia ukwepaji wa kodi ( Magendo)
VIONGOZI TRA.jpg

WAOMBOLEZAJI.jpg
 
Wote ni mavumbi na tutarudi mavumbini

Kauli ya KIFO NI KIFO TU naendelea kuitafakari!
 
TRA mnatakiwa kufanya kazi zenu kwa kufuata taratibu na sheria za nchi. Ninaamini kabisa kama mngefuata utaratibu, hili tukio lisingetokea. Hivyo mjifunze kutokana na makosa.
 
Waziri wa fedha Dr Mwigulu Lameck Nchemba leo tarehe 8/12/2024 ameongoza waombolezaji na ndugu wa marehemu Amani Simbayo katika kutoa heshima za mwisho kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Malinyi kwa ajili ya mazishi.

Soma Pia:
Katika hotuba yake Mhe Waziri Mwigulu amisisitiza wananchi kutokujichukulia sheria mikononi na kusikitishwa na kitendo kilichopelekea kifo cha Amani.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila amekemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi kujihusisha na vitendo vya kujichukulia sheria mikoni na kusema kuwa vipo vyombo husika vilivyopewa dhamana ya kusimamia sheria.

Kwa upande wake Kamisha Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Yusuph Mwenda amewapa pole wafiwa na kusema TRA itaangalia namna ya kumsaidia mjane pamoja na watoto wa marehemu.Amesisitiza kuwa marehemu alikuwa kwenye majukumu yake kwa mujibu wa sheria na ameuwawa akiwa anatekeleza majukumu yake kusimamia ukwepaji wa kodi ( Magendo)
Siku hizi kila mwenye madaraka au cheo anakuwa juu ya Katiba, sheria, kanuni na taratibu halali.

Marehemu ni victim wa makundi mawili
  1. Mobjustice ya wananchi waliochoshwa na utekwaji nyara na hata victims kupatikana maiti. Wananchi wanatumia mob justice kujilinda na hii itasambaa sana
  2. Some irrelevant responsible leaders ambao wanapuuzia matukio ya utekwaji nyara, jeshi la polisi linalotumia mbinu za kigaidi kukamata raia bila kujali haki, taratibu na sheria zilizopo. Utaratibu uliotumiwa na TRA pale Tegeta kwa Ndevu ni wa utekaji nyara. Hawakumsubiri mtuhumiwa apaki waweze kumdaka wao walimvamia kama muuaji vile.
TIP
Ukiangalia picha ya msibani, maswali ni mengi zaidi ya kinachoonekana hapo.

Tumpe nafasi marehemu aikabili hukumu yake ya kaburi. Cha kusikitisha irresponsibles wamemgharimu uhai wake.

Kumbe watekaji wana familia na unaona wapo innocents kama walivyo wanafamilia wa watekwaji. Basi kila.mmoja athamini ukweli na uwepo huo
 
Back
Top Bottom