Wakuu,
Mbona mambo yanazidi kukorogwa! Aliyeelewa hapa aniaeleweshe!
====
Wakati Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akidai mgombea ujumbe wa chama chake Mtaa wa Ulongoni A, Modestus Timbisimilwa kuwa ameuawa kwa kupigwa risasi na Polisi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema amefariki kwa shinikizo la damu.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Katika chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii leo Novemba 27, 2024 Mbowe ameandika:
“Tunapofunga vituo vya kupiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Taifa limeendelea kushuhudia tena ubaradhuli wa wazi na wa aibu toka kwa mamlaka zote za Serikali kushirikiana kuipatia CCM na wagombea wake ushindi wa aibu hata kwa gharama za maisha ya Watanzania.
Pia soma: LGE2024 - TANZIA - Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024
“Tunalaani mauaji na kujeruhiwa kwa wagombea, viongozi na wanachama wetu mbalimbali wakiwemo: Modestus Timbisimilwa, mgombea nafasi ya ujumbe wa serikali ya mtaa wa Ulongoni A, Kata ya Gongolamboto, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam aliyeuwawa na askari kwa kupigwa risasi wakati wa purukushani za kuzuia kura bandia na batili kuingizwa kituo cha kupiga kura.”
Alipoulizwa Kamanda Muliro kuhusu tukio hilo pamoja na matukio mengine amesema mgombea huyo amefariki kwa kuugua presha na kinachosambazwa mitandaoni hakina ukweli.
PIA SOMA
- LGE2024 - Manyoni: Jeshi la Polisi linamshikilia Askari aliyesababisha kifo cha mgombea wa CHADEMA, kama kawaida risasi imekata kona!