Dar es Salaam ikifika usiku ndugu nenda kalale, watu wanakufa sana usiku halafu nashangaa haitangazwi

bongo man

JF-Expert Member
Dec 26, 2016
1,053
2,338
Habari za usiku ndugu zangu, nami nikaona kabla sijapatwa na usingizi niweke hapa uzi wa uzeofu wangu kuhusiana na maisha ya Dar es salaam usiku. Shuhuda vifo vya ajabu; ajali, visa na mikasa.

Ndugu zangu mimi ni mkazi wa Dar, nimezaliwa Dar na kukulia Magomeni mtaa wa Kizingo nyumba no (siri) kwa wale wanaokujua vizuri watakuwa wanapapata, nimeenda shule kidogo kuondoa ujinga baadae nikaanza kujichanganya na shughuli mbali mbali.

Kama ufundi umeme, udereva wa boda, boda mwanzoni kabisa sio sasa kelele nyingi, udereva tax na udereva wa tipa za mchanga kabla sijaamua kujiingiza katika biashara na kilimo huku mikoani ambako ndio naishi hadi leo.

Samahani kwa kuwachosha wazee, twende kwenye mada sasa.

Ndugu zangu nimehangaika sana mikoa hasa majiji makubwa kama Arusha, Mbeya, Mwanza n.k yote katika kusaka maisha ila sijawahi ona jiji lenye vurugu na vifo vya kutisha vya usiku kama Dar es Salaam.

Tuanzie miaka ya 2005 ndio namalizia coz yangu fupi ya ufundi pale Veta_Chang'ombe, nikaangia mtaani kuzisaka noti, wazee nilikuwa nikapata kubarua kwenye kikampuni flani cha matangazo kinadeal na kubandika matangazo kwenye nguzo za barabarani, hivyo kwa nafasi yangu kama fundi umeme ni kuweka installations ili usiku mwanga uwake tangazo lionekane vyema. Kampuni ilikuwa Kurasini, sasa hii kazi haina muda maalumu supervisor akipita kukagua matangazo akikuta taa haziwaki lazima uamshwe ukawekee mambo sawa aise.

Sasa lazima uchukue pikipiki uende usiku kuanzia saa nane mpaka tisa nilikuwa nakutana na visa njiani vya kutisha, ajali barabarani tena maiti zipo kwenye gari zinatoa damu kabisa ila tunapita tu tunaendelea na yetu aisee wakati mwingine utakuta maiti ya mlevi au mwanamke ipo pembezoni mwa barabara unaipita tu unaendelea, hii waliofanya bodaboda za usiku watakuwa mashahidi humu cha ajabu kukikaribia kucha hukuti maiti wala nini hata gari za ajali ilikuwa mara chache kuzikuta bado zikiwa barabarani halafu hakuna chombo chochote wala taarifa ya habari inayotangaza hayo matukeo sijui kwanini hadi sasa haya matukio yalikuwa yanatokea mara nyingi kati ya barabara ya kuelekea Aga khani na hii ya kutokea Muhimbili na surrender bridge aise kila nikienda site usiku lazima nipishane na maiti au ajali za kutisha.

Miaka ikaenda nikaachana na kazi ya ufundi nikanunua bodaboda yangu ndio kipindi zinaingia, nikanunua chuma kwa mtaji wa kudunduliza nikawa na kijiwe changu pale Lego hotel Sinza sina unakika kama bado ipo ile hoteli nikaanza kuzungusha abiria kama sina akili. Kazi enzi hizo zinalipa usiku mchana ni kulala tu mjini tu aingia muda wote wote sio sasa mpaka Makonda acheke khaa. Mzee sasa ndio nikawa mzoefu wa kuona mambo ya ajabu watu wanagongwa usiku magari hayasimami, maiti inarushwa mbali hakuna anaejali hasa kipindi vijana wengi ndio wameanza kuendesha bodaboda kila siku ilikuwa lazima nione maiti za waendesha pikipiki na walevi zinagongwa zipo barabarani hasa maeneo ya maeneo Manzese darajani na Magomeni mataa watu walikuwa wanakufa aise hadi nikaanza kufikiria kuachana na kazi hiyo ya bodaboda aise kwenye taa gari inakupita anakubaramia kama vile wewe si binadamu na huo anaondoka Zake hizo mambo nimezishuhudia zaidi ya mara tano kwenye round about mbali mbali watu wanapigwa tena wamesimama kwenye taa.daahhh maishaa...

So maisha yakawa yanasonga baadae nikawa tanboy kwemye tipa za mchanga baada ya blaza kupata gari la mchanga la kutoa material Lugoba na Bagamoyo kuingiza mjini miaka ya 2013 aise hapo ndo nipo niliamini kuwa Dar es salaam watu wanakufa aise baada ya kukaa utanboy miaka 2 nami nikawa mzoefu basi blaza anakoma na kazi za mchana nami ananipa trip za usiku kuingiza mchanga usiku mjini

Nachukua mchanga bagamoyo naenda kupaki bunju nasubiri isiku uingie niingize matrial mjini basi maisha yakawa ndo jayo lwa miaka 4 nikawa silali usiku. Usiku moja nilishuhudia ajari maeneo ya red cross nyuma kidogo ya chuo cha english fountain opposite na las vegas wahindi wametokea kula bata na mademu zao wakaingia barabara ya kuingia upanga ya vumbi kumbe wakati wanaingia barabarani hawakuona nyuma aise ilitokea coaster tupu iliwachana na kigari chao aise kwa mara ya kwanza nikashuhudia jicho la binadamu na linaninga'inia kwenye mirror ya mbele aliekaa nyuma kabanwa kichwa kimepasuka ubongo unatiririka ka.a maziwa aiseee niliogopa sanaa halafu hakuna mtu sisi ndo tulikuwa tumefika sites ya jirani tukaenda kuangalia aise niriludi mwenyewe bila kusema chochote na tanboy tukamwaga mchanga tukaondoka zetu.

Miaka ikasonga nikafanikiwa kununua ki corona changu nikawa napaki africa sanaa nikawa nashuhudia unyama sasa kubakwa kwa machangudoa ,watu kulishwa madawa na kukimbiwa .mademu kutembea uchi wa mnyama kabisa kufanya ngono zembe hadharani kabisa maisha yakawa ni vurugu tupu kwakweli si mshauri mtu kufanya shughuri za usiku Dar hakufai aise. NIWAOMBE NDUGU ZANGU IKIFIKA USIKU DAR NENDA KALALE USIKU HAKUNAGA MSAADA MTOA RIZIKI NI MOLA TU..SHUKRANI
 
Kuna kipindi niliwahi kuendesha daladala, ukizingatia sikuwa na leseni basi nikawa naendesha usiku tu(kuua paka, kuwanga)

Gari lenyewe lilikua mkweche, basi ni ruti yoyote utakayoona kuna abiria unaenda, iwe buguruni, kkoo, mbezi shamba, tegeta, mbagala popote pale tulikua tunaenda, mpaka kunakaribia kukucha unajikuta umeizunguka dar yote.

Naungana na mtoa post, jamani dar watu wanakufa sana usiku, sio siri, mfano njia ya bunju mpaka mwenge, kila ninavyopita ni lazima nikute ajali zaidi ya moja, yaani nikiwa naenda mwenge nakuta ajali kama tatu au nne, na nikiwa narudi tegeta siwezi kukosa kuona ajari walau mbili, kuna hiki kipande kati ya mataa ya mbezi shule na kituo cha kwa komba, aisee eneo karibu kila siku ilikua ni lazima nione ajari, yaani ilifika kipindi nikawa nikiona ajari namwambia konda wangu "kila siku tunaona za wenzetu, ipo siku na watu wataona ya kwetu"

Yaani ilikua tukipita bila kuona ajari basi konda ananitazama na mie namtazama kisha ataniambia "au leo ndio zamu yetu nini?" jamni watu wanakufa sana dar usiku.

Njia ya mbezi nayo si haba kwa ajari, buguruni ndo kabisaaaa matukio na ajari ni kama yote.

Nakumbuka kuna siku tuliwahi kujaza mafuta kituo flani hivi, sasa baada ya kumaliza kujaza mie nikaanza kuendesha gari, kumbe konda hakua amelipa hela(halafu aliepewa kazi ya kujaza hakuwa muhusika mkuu, alikua ni masai mlinzi ndo alitujazia) basi gari ikiwa imeanza kuingia barabara kubwa, yule masai ndio akaanza kuikimbilia apewe hela(mie hapo sina habari) nikatembea na ukali bwana bwanaaaa!

Yule masai akaita wezi weziii wameiba mafuta, mamamamaaaa, yaani boda boda wote waliokuwa pale wakawasha vyombo kutufukuzia, hapo sio mie wala konda ambae ana habari kuwa tunafuatiliwa, yaani ile napaki tu kituoni naona maboda boda yametuzunguka, fastaa nikachomolewa na kipigo, konda akafunga mlango wakavunja kioo wakamtoa na hela yooote wakachukua, p

pona yetu alikua ni yule masai kufika mapema eneo la tukio, baada ya kuhojiwa akajieleza, na konda alipoulizwa akasema, yeye masai alipomaliza kujaza aliondoka keenda chooni bila kuchukua hela, hivyo akawa anamtafuta so wakati anamtafuta mimi ndio nikaanza kutoa gari so akaamua kudandia huku akiendelea kuangaza, na masai alipoona gari inaondoka ndio akaanza kuikimbilia, konda alipomuona masai akaamua kumtupia ile hela chini maana gari ilikua inaondoka, masai hakuelewa kama hela imetupwa so akaita weziii.

Ilitubidi tugeuze mpaka kule kwenda kuitafuta ile hela mpaka ikaonekana ndo ikawa pona yetu la si hivyo tungechomwa moto na daladala yetu.

Kurudi kumueleza bosi sababu ya vioo kupasuka haelewi, yeye anasema eti kulibeba majambazi kwenda kufanya tukio hivyo kulikurupushwa na wananchi ndo wakavunja vioo, akataka hesabu tukamwambia tuliporwa ndo akazidi kuwa mbogo, nakumbuka ilivyofika saa moja asubuhi, badala ya kwenda kulala vitanda. vya nyumbani, usingizi ulitukuta tukiwa ka seroo kadooogo(in kali p voice)
 
Back
Top Bottom