Kumekuwa na changamoto ya ajira,ongezeko la maji taka, na upungufu katika vyanzo vya maji yaliyokuwa yanatumika kwa kilimo. Nadhani imefika wakati sasa serikali kuunganisha hoja hizo na kutoa suluhisho. Wazo la kurudia kuyatumia maji baada ya matumizi ya awali ndilo linalofanyiwa utafiti kote duniani kwa sasa.
Kwa Dar ,hili litawezekana iwapo, wahusika mbali mbali, kuanzia mipango miji hadi watu wamamlaka za maji safi na maji taka wakiungana na kutoka na mradi wa pamoja. Nchi kama jordani, uholanzi, australia na nyinginezo zinafanya. Kuna maeneo wamekuwa wakilima mboga mboga hapa mjini bila kutibu maji husika. Njia kama wastewater stabilization ponds na constructed wetlands zinaweza kutumika kupunguza gharama. Nimeambatanisha study kwa wale watakao guswa. Najua hili wazo linchangamoto zake, ila zikijadiliwa na kufanyiwa utafiti nadhani itatusaidia.