Dar es Salaam bado ni jiji la kimasikini saana! Ushahidi kwenye picha!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
5,870
16,819
Hii picha imepigwa kutoka PSSSF tower floor ya 33. Angalia vijumba zaidi ya 99% viko chini! Hii inaonyesha kiwango cha juu cha umasikini na ustawi wa jiji la Dar es Salaam! Tunataka tuwe megacity yenye skyscrapers kama New York!
downloadfile.jpg
 
Hii picha imepigwa kutoka PSSSF tower floor ya 33. Angalia vijumba zaidi ya 99% viko chini! Hii inao nyesha kiwango cha chini cha umasikini na ustawi wa jiji la Dae es Salaam! Tunataka tuwe megacity yenye skyscrapers kama New York!
Mkuu umasikini haupimwi kwa kujaza magorofa mjini, neenda London uone kama kuna skyscraper kama zilioko Cairo au Dubai
 
Hii picha imepigwa kutoka PSSSF tower floor ya 33. Angalia vijumba zaidi ya 99% viko chini! Hii inao nyesha kiwango cha chini cha umasikini na ustawi wa jiji la Dae es Salaam! Tunataka tuwe megacity yenye skyscrapers kama New York!View attachment 3168527
Mbona ni eneo moja tu ambalo umepiga picha tena kwa juu? Hapo ni Sinza Palestina sasa ungeenda barabara kuwa ya shekilango ukapiga picha tuone nako . Ukinaliza nenda Kigamboni, Bunju, Makongo, Mbweni, Mbezi zote mbili, Mikocheni, Magomeni, nako tuone walau kukoje.
 
Hiyo ndiyo raha ya mtu ambaye ndio mara yake ya kwanza kuwa juu ya jengo refu.
Usimshangae!
 
Tajiri mwenye akili lazima ajenge ghorofa mjini maana ni matumizi bora ya ardhi. Kwani uchumi wewe ulisomea nchi gani, mkuu?
Sio lazima kujenga ghorofa,kuna njia kibao tajiri anaweza invest hela zake...au haujui Dar kuna maghorofa mengi hayana wapangaji?utaona tu mabango yameandikwa"TO LET 0780 448 899"Huoni haya magorofa ni white elephant project?nenda kwenye magorofa ya serikali yapo ya magorofa kibao hawaishi watu huo ni ujanja au ujing.a?
 
Tajiri mwenye akili lazima ajenge ghorofa mjini maana ni matumizi bora ya ardhi. Kwani uchumi wewe ulisomea nchi gani, mkuu?
Siyo lazima kila maeneo kujenga magorofa na siyo lazima kujenga gorofa sababu wewe ni tajiri. Sasa eneo la makazi unajenga gorofa 35 unaishi na watoto 3 la nini? Nenda upanga ndiyo utakutana na magorofa sababu ni eneo lililotayarishwa kwa ajili hiyo.
 
Hii picha imepigwa kutoka PSSSF tower floor ya 33. Angalia vijumba zaidi ya 99% viko chini! Hii inao nyesha kiwango cha chini cha umasikini na ustawi wa jiji la Dae es Salaam! Tunataka tuwe megacity yenye skyscrapers kama New York!View attachment 3168527
Umeleta kihoja mkuu wala siyo hoja hii! Umaskini unaupimwa kwa kuangalia maghorofa? Una mawazo ya kitumwa sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom