Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 25,426
- 18,858
Ndugu zangu Watanzania,
Inaumiza sana, inasikitisha, inahuzunisha, inatia hasira, inaleta simanzi, inasononesha na kuleta uchungu mkubwa sana ndani ya Moyo kuona, kusikia, kutizama, kushuhudia na kupata habari kuwa kuna watu, watanzania wenzetu,wenye mioyo ya nyama na Damu.
Wanaweza kufanya ukatili, uovu, ushetani na unyama wa kiwango cha namna hii cha kuteka na kuuwa na kukatisha maisha ya mtoto mdogo kama huyu asiye na hatia na Malaika mbele za Mungu.
Damu ya huyu Mtoto haitaenda bure, haijamwagika na kunyamaza kimya. Ni kweli amelala kwa maumivu makubwa usingizi wa milele, lakini Damu yake inanena na Itazungumza na kuwaonyesha watu wate na mtandao wote waliohusika katika kukatisha maisha ya Mtoto huyu popote pale watakapo kuwa.
Damu ya mtu asiye na hatia inayomwagwa na watu ardhini pasipo na kosa wala hatia haijawahi kunyamaza wala kukaa kimya hata mwili ukiwa umelala ardhini na kufukiwa na udongo. Damu inayomwagwa bila hatia inakawaida ya kuzungumza ukweli, kunena bila uoga wala hofu na kulipa kisasi na kutoa au kuacha laana kwa mikono yote iliyohusika kuimwaga chini.
Mtoto huyu amelala, amelala usingizi wa milele, amelala kwa sababu ya ukatili na roho za kikatili na kinyama za baadhi ya wanadamu,amelala kwa maumivu,amelala kwa kifo cha mateso.
Nenda Mtoto, Lala salama, Mungu akuangazie Mwanga wa Milele lakini Damu yako itaendelea kunena na kuzungumza mpaka wote waliokutesa na kukukatisha uhai wako kwa mateso wapatikane wakiwa hai au wamekufa.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Pia soma: Kufuta mauaji ya albino, ni kutokomeza kabisa Waganga wapiga ramli