Nipe Maji
Member
- Mar 25, 2025
- 66
- 43
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro
amesema kuwa, Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia mpaka sasa imefika katika mikoa 23, ambapo imesikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi ambapo mpaka sasa takribani wananchi milioni mbili, laki moja na tisini na mbili, mia tatu sabini na mbili wamefikiwa na Huduma za Msaada wa Kisheria.
Akiwahutubia Wananchi waliofika kwa ajili ya kushiriki katika uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika katika viwanja vya Ngarenaro jijini, Arusha Waziri Ndumbaro amesema kuwa mpaka sasa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Arusha, imefika kwenye Halmashauri 154, Kata 1,639 na vijiji takribani 4,897.
Akisisitiza malengo ya Kampeni hiyo iliyoasisiwa na kufadhiliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Ndumbaro amesema lengo lake ni kutoa Msaada wa Kisheria kwa Wananchi hususani wanyonge na wale wa pembezoni wasiofikika kirahisi pamoja na kutoa Elimu ya Sheria na Haki za binadamu, Elimu ambayo imetolewa pia kupitia vyombo vya habari na kuwafikia Wananchi Milioni 43 tangu kuanza kwa Kampeni hiyo.