Dalili nane za kuonyesha unaishi kwenye malango yaliyofungwa (closed gates) katika ulimwengu wa roho

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,793
15,277
ZIFUATAZO NI BAADHI YA DALILI NANE MUHIMU ZINAZOONYESHA KUWA MALANGO YAKO YAMEFUNGWA NA ADUI🦸🦸🦸

1. UNAPOTEZA KIBALI NA BADALA YAKE UNATAWALIWA NA ROHO YA KUKATALIWA(SPIRIT OF REJECTION).
Inawezekana ikawa kwenye ndoa,uchumi, biashara,uzao,afya,familia,uchumba,kazi,siasa,uongozi(utawala).
Ukiona haupati kibali na unakataliwa basi ujue malango yako ya hiyo sehemu yamefungwa na wachawi.

2.KILA UANZALO KULIFANYA UNAJIKUTA HALIFIKII MWISHO WA UTUKUFU(LINAISHIA NJIANI)
Haijalishi ni biashara,kazi,mradi,kampuni,ndoa,familia,
Na mahali penginepo unashangaa unaanza vizuri lakini unaishia njiani(hauoni kuufikia mwisho wa malengo).

3.KUJIRUDIARUDIA KWA CHANGAMOTO AU TATIZO LINALOFANANA LINALOPELEKEA KUKUZUIA KUSONGA MBELE.
Changamoto hiyo inaweza kuwa ni kuanguka kwa mtaji,
Kuongezeka kwa madeni,ugonjwa,kuibiwa,kufilisiwa,kutapeliwa,kuachika,kufukuzwa,kuaibishwa,
Hali ambayo inajirudiarudia kila mara kwenye eneo hilo.

4.KUKUTANA NA VIZUIZI(VITA KALI) AMBAVYO INAPITA UWEZO AU NGUVU ULIZONAZO.
Ujue kwamba adui akifunga malango anao uhakika wa kwamba huwezi kuvuka kwa namba yoyote ya kibinadamu
Yaani akili zako,nguvu zako Wala uwezo wako.
Yaani vinginevyo Mungu mpaka aingilie kati.

5.JITAHADA YA NGUVU UNAZOTUMIA HAZIENDANI NA MATOKEO UNAYOPATA.
Yaani ni sawa na kupata hasara
Maana unajikuta unatumia nguvu kubwa lakini matokeo madogo,
Kuna waswahili wanasema
"Nguvu tembo,matokeo sisimizi,)

6.HUONI MIPENYO(BREAKTHROUGH)
KWA MUDA MREFU.
Yaani wakati wengine wanafanya hichohicho unachokifanya wanafanikiwa na kuongezeka,
Wewe ndio kwanza unarudi nyuma(backsliding) na muda unazidi kupotea.
🤔🤔

7.KILA MIPANGO YA MAFANIKIO UNAYOPANGA UNAJIKUTA INAHARIBIKA KABLA YA KUITEKELEZA.
Inaweza kuwa mipango ya ndoa, biashara,kazi ,uchumi,familia ,huduma,na mahali penginepo
Unajikuta inaharibika kabla ya kutekelezeka.

8.KUTAWALIWA NA MADENI YASIYO NA SURUHISHO....
Hapa ninamaanisha madeni ambayo ulipokopa unajikuta hufanyii mambo ya maana na kila ukijitahidi kuyaondoa inashindikana...
Na zaidi yanakusukuma kwenye utumwa mkubwa wa nafsi pasipo suruhisho lolote penginepo badala ya kupungua ndio kwanza yanaongezeka....🤔🤔

9.UNAKUWA UNAOTA NDOTO MBAYA ZA KUTISHA,😒😒😒
Mfano wa ndoto hizo ni kama zifuatazo:

✍️ Unakuwa Unaota unafukuzwa na wanyama wakali (wakiwemo ng'ombe).
✍️Unakuwa Unaota unaishi vijijini ulikozaliwa wakati kwa uhalisia hauishi huko.
✍️Unaota unazini na watu unaowafahamu na usiowafahamu.
✍️Kuota unasoma shule ya msingi au sekondari wakati kwa uhalisia ushapita huko.
✍️Unakuwa Unaota unatembea pekupeku(bila viatu)
Wakati mwingine Unaota uko uchi kabisa.
✍️Unaota umedumbukia chooni au kwenye shimo au unaishi chooni kabisa.
✍️Unaota unanyonyesha watoto wakati kwa uhalisia hauna mtoto mdogo.
✍️Unaota unanyolewa nywele.
✍️Unaota unazikwa ingali uko hai
Wakati mwingine jeneza linapita mbele Yako.
✍️Unaota unatolewa damu hospitalini.
✍️Unaota unakula chakula.
✍️Unaota unashirikiana na watu waliokufa.

Hizo ni baadhi ya ndoto.

10.Wengine wakiota ndoto wanapoamka asubuhi hawakumbuki chochote kabisa,
Nayo hiyo ni dalili ya malango Yako ya baraka kufungwa.
 
Tusahidie tunatokaje Sasa au inaisha automatically?
Suluhisho ni nini sasa mkuu?
Suluhisho ni kukesha na kuomba ulinzi wa Mungu sali na soma biblia mara tatu unapoingia kulala kemea kwa damu ya YESU soma
Zaburi 91:1-5
Kila siku unavyoingia kulala
hizi ndoto mbaya zinazojirudia rudia mara nyingi vunja laana na mikosi ya maagano ya ukoo kwa damu ya YESU usisahau kuamka saa kumi usiku kuomba ulinzi wa Mungu bila kuamka usiku imekula kwako

Ukiona inaanza kuota ndoto upo kanisani au upo na wachungaji ujue hizi ndio ndoto njema
Kama unaota ndoto za kula basi hakikisha unakula matunda au maziwa
 
Nini maana ya malango? Na yanafungwa kivipi? Tafadhali naomba ufafanuzi!
 
ZIFUATAZO NI BAADHI YA DALILI NANE MUHIMU ZINAZOONYESHA KUWA MALANGO YAKO YAMEFUNGWA NA ADUI
Watu wengi sana wamefungwa, wapo ndani ya magereza yenye "maximum security" bila kujua watamaliza vipi na lini kutumikia mateso na vifungo vyao.

Ndiyo sababu akitokea mtu akasema ana suluhisho kama Bulldozer, Musa, nk, wanapata wateja wengi kuliko hata hospitali, nk.
 
Suluhisho ni kukesha na kuomba ulinzi wa Mungu sali na soma biblia mara tatu unapoingia kulala kemea kwa damu ya YESU soma
Zaburi 91:1-5
Kila siku unavyoingia kulala
hizi ndoto mbaya zinazojirudia rudia mara nyingi vunja laana na mikosi ya maagano ya ukoo kwa damu ya YESU usisahau kuamka saa kumi usiku kuomba ulinzi wa Mungu bila kuamka usiku imekula kwako

Ukiona inaanza kuota ndoto upo kanisani au upo na wachungaji ujue hizi ndio ndoto njema
Kama unaota ndoto za kula basi hakikisha unakula matunda au maziwa
ni saa 9 usiku,usisahau kuogea chumvi ya Mawe.
 
Mbona ni vitu vya kawaida katika hali ya ubinadamu... ni sehemu ya maisha hamukawii kusema kuna dawa.. hii ni nature kwa viumbe.. hata mbwa anaota.. ukute hata sleep paralysis mtaita uchawi/nguv za giza.. hahahahahah science
Mtu anakuwa hana commitment kwenye mipango yake, anakuwa mvivu, anakopa madeni yasiyo na mipango, huna malengo, hujichanganyi au hutafuti connection kwa watu, huangalii ni wapi ulikosea kwenye maamuzi au machagua yaliyopita ukajirebisha, unasingizia kuna mtu kafunga milango yako kwa nguvu za giza kweli.
 
Back
Top Bottom