johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,124
- 164,525
Niwapongeze wamiliki wa daladala za Tegeta Nyuki - Kivukoni kwa kuanzisha mfumo wa malipo ya nauli kielektroniki, lakini pia kwa kuanzisha mfumo wa malipo ya nauli kwa kutumia kadi maalumu. Kadi hiyo ( smart card) inauzwa sh 500 tu na baada ya hapo unaingiza salio ambalo utatumia kulipia nauli kila unaposafiri. Leo nimesafari na moja ya daladala hizi na kushuhudia abiria wengi wakilipa nauli kwa kutumia kadi. Itapendeza zaidi kama na route nyingine za daladala zitafuata mfumo huu. Nawasilisha!