KERO Daladala za Kilombero - Kiseriani (Arusha) hukatisha ruti kuanzia Saa 1 Usiku na kusababisha usumbufu kwa abiria

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

miguu ya kuku

Member
Jan 14, 2025
6
8
Kumekuwa na tabia ya Daladala nyingi zinazofanya safari za Kilombero - Kiseriani kuwa na tabia ya kukatisha ruti kuanzia majira ya Saa 1 Usiku na kusababisha abiria kupata adha ya usafiri wakati wa usiku kwani nusu nzima za Haisi huanza kuishia Moshono Kona.

Hali hiyo husabanisha abiria wengine kuning'inia nyuma na mlangoni na nyuma ya buti kutokana na uchache wa Haisi, hivo kuhatarisha maisha yao.

Tunaomba Viongozi na mamlaka zinazohusika ikiwemo LATRA mlishughulikie hili suala limekuwa likiathiri watu wengi wanaopanda daladala katika njia hiyo.

Pia soma Makonda wa Arusha ruti ya Kilombero kwenda Kiseriani Madukani wanaibia abiria nauli

IMG_20250111_205818_285.jpg
IMG_20250111_205908_015.jpg
IMG_20250113_195812_299.jpg
IMG_20250113_202213_699.jpg
IMG_20250113_202217_276.jpg
 
Back
Top Bottom